` MISA TAN NA WADAU WA HABARI WAENDESHA MJADALA KUKABILI HABARI POTOFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

MISA TAN NA WADAU WA HABARI WAENDESHA MJADALA KUKABILI HABARI POTOFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025


MISA Tan , PACJI, MYCN na CILAO yaendesha mjadala juu ya habari potofu kuelekea uchaguzi Mkuu 2025

Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania( MISA TAN) Kwa kushirikiana na Taasisi ya Pan African Constructive Journalism Initiative, CILAO na MYCN zimeendesha mjadala wa kimtandao wa kijadili athari za habari potoshi kuelekea uchaguzi Mkuu 2025.

Mwenyekiti wa MISA Tan Edwin. soko alisema kuwa, mijadala kama huo walioandaa ni muhimu kwenye kuwaandaa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

"MISA Tan Kwa kushirikiana na wenzetu Taasisi ya PACJI, MYCN na CILAO tumeona hatari ya kuwa na habari potofu kuelekea uchaguzi mkuu 2025 na hivyo kuona umuhimu wa kuandaa mkutano huo ili kujadili namna na kupunguza habari potofu,"amesema Soko.

Ameongeza kuwa MISA Tan itahakikisha mijadala hiyo inakuwa uendelevu na Kwa hatua zijazo watajitahidi kuandaa kongamano la kitaifa la waandishi wote ili wakutane na kujadili Kwa kina .

Naye Mwenzeshaji Mary Kafyome alisema kuwa, uchaguzi wa Mwaka hiuu utagubikwa na matumizi makubwa ya teknolojia hivyo ni lazima hatua zichukukiwe mapema dhidi ya habari potofu.

Naye Mzungumzaji Odero. Odero alivitaka Vyombo vya habari kujua sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya uchaguzi ili viweze kufanya kazi Kwa weledi.

Naye Mzungumzaji Abishagi Bhoke alisema kuwa ili kuepuke kutolea kwa habari potofu ni muhimu kuielikisha jamii juu ya matumizi sahihi ya mtandao.

Naye Mshereheshai wa mkutano huo Daktari Dotto Bulendu alisema kuwa, wadau wa uchaguzi ni muhimu Kwa sasa kukaa Kwa pamoja na kujadili changamoto hizo za habari potoshi kuelekea uchaguzi mkuu.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bwana Rodney Thadeus alifunga mkutano huo wa mtandaoni Kwa kuwataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya taaluma yao wanapotekeleza majukumu yao.

Thadeus pia aliwashukuru waandaji Wakuu wa mkutano huo wa kimtandao Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, Tawi la la Tanzania, Pan African Constructive Journalism Initiative (PACJI), CILAO na Mwanza Youth and Children Initiatives (MYCN) na washiriki wote wa mkutano huo Kwa kujitokeza na kushiriki mkutano huo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464