
Bosi alinitaka kimapenzi ili kunipandisha cheo ila nikamkataa
Kusema kweli nikiwa kama dada ninayepambana, itanichukua miaka mingi sana kuja kusahau kitendo cha Bosi wangu niliyekuwa namuheshimu sana alipoaniambia ili kupanda cheo kazini basi ni lazima nilale na angalau mara mbili.

Nilikataa mara moja kwani uwezo wa kazi ninao mzuri na isitoshe nimesoma vizuri na vyeti vya kitaaluma ninavyo. Nikajisema kimoyo moyo kama vipi nitaacha hii kazi akiendelea kunisumbua kuhusu jambo hilo.