` NHAMANILO AONGOZA KONGAMANO LA UWT WILAYA KWA KISHINDO KIKUBWA, HUKU VIONGOZI WAKE AKIWATAKA KUWA WAADILIFU NA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE MAADILI YA UONGOZI BORA

NHAMANILO AONGOZA KONGAMANO LA UWT WILAYA KWA KISHINDO KIKUBWA, HUKU VIONGOZI WAKE AKIWATAKA KUWA WAADILIFU NA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE MAADILI YA UONGOZI BORA


Suzy Butondo, Shinyanga

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo ameongoza kongamano kubwa la wanawake wa UWT kuanzia ngazi ya matawi hadi kata kwa lengo la kuwapa elimu ya maadili katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu.

Kongamano hilo limefanyika mjini Shinyanga , ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Anold Makombe, na katika kongamano hilo mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi alifika kusalimiana na kuwashukuru viongozi wa UWT kwa kuendellea kushirikiana.nae katika kufanya maendeleo

Nhamanilo amesema wameandaa kongamano hilo kwa ajili ya kuwapa elimu ya maadili viongozi kuanzia ngazi ya matawi na wilaya katika kuelekea kipindi cha uchaguzi,ambapo aliwaomba viongozi wote kufanya uchaguzi sahihi wa kuwachagua viongozi sahihi wenye maadili ya uongozi.

"Tuliona sio vyema tukutane tu kwenye uchaguzi, tukaona ni vizuri tuandae kongamano hili ili kukutana na viongozi wote wa matawi kata na wilaya tupeane elimu ya maadili ili tunapoingia kwenye uchaguzi tuwe tunajua kiongozi mwenye maadili ni yupi,nani anaweza kutuwakilisha kupitia kwa madiwani na mbunge"amesema Nhamanilo.

Aidha watoa mada wa kongamano hilo ambao walitoa mada mbalimbali zikiwemo za ukatili wa kijinsia,
Takelove Ayo kutoka Polisi Dawati la jinsia, ...kutoka Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Shinyanga mjini na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha ambaye alizungumzia maadili ya kiongozi.

Chacha amesema kiongozi mzuri anatakiwa kuhakikisha kuwa wale anao waongoza wanajivunia yeye kwa maana akisimama mbele yuko tayari kuwaongoza na kuwasemea ipasavyo kama hafanyi hivyo ni kiongozi ambaye atamaliza muda wake bila kufikia matarajia wala mafanikio malengo wanayoyatarajia kutoka kwake.

"Sisi kama wanawake tunalojukumu kubwa la kuisaidia jamii na kuhakikisha viongozi tunaowachagua ni wale ambao wanaenda kutuletea mafanikio makubwa ambayo yatamuwezesha mwanamke kutekeleza majukumu yake kwa urahisi zaidi kwa sababu ukizungumzia huduma za afya wanawake ndiyo wahusika wakubwa wanapeleka watoto wanapeleka waume zao na wanaenda wao wenyewe hivyo tunahitaji kiongozi bora atakayewawakilisha wanawake na wananchi wote"amesema Chacha.

"Kwa kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi ni vizuri kiongozi awe na maadili ya kiuongozi yanatakiwa yaonekane mbele ya wale unaowaongoza,hata kucheza unatakiwa uwe na staha, na kiongozi mzuri hutakiwi kunywa pombe za kupita kiasi,hutakiwi kusutwa popote kuanzia kwenye mtaa wako, hutakiwi kushikwa ugoni,wewe kama kiongozi, unatakiwa uwe mfano kwa watu unaoishi nao,ili wanawake waendelee kuaminika"ameongeza Chacha.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi amezungumza na wanawake wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini na kuwaomba wafanye uchaguzi sahihi katika uchaguzi mkuu ili kuwachagua viongozi bora wenye maadili na wenye kutatua kero mbalimbali zilizopo kwenye jamii.

Katambi amesema anawashukuru viongozi wote kwa kushirikiana nae katika kutekeleza miradi ya maendeleo aliyokuwa ameiahidi kuitekeleza katika kipindi cha miaka mitano kwa kushirikiana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

"Tumefanya kazi katika kipindi kigumu lakini mmekuwa pamoja nami, ahadi zote nilizoahidi tumezitekeleza, kwa msaada wa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan hatua tuliyoipiga yote tumetekeleza,tumetengeneza barabara na sasa tuna mpango wakutengeneza barabara za lami kata kwa kata"amesema Katambi.

"Wanaopata shida ni wakina mama na watoto, hivyo barabara ya Mwawaza inayoelekea katika hospitali ya rufaa ya Mkoa inaenda kutengenezwa kwa kiwangocha lami,kwani matamanio yangu ni kuona manispaa yetu inakuwa na maendeleo makubwa na tunatamani kuwa na vyuo vikuu vinaongezeka,hivyo tunahitaji kupata uongozi bora"ameongeza Katambi.

Hata hivyo Katambi baada ya kuzungumza na viongozi ametoa vifaa vya kutotoresha kuku ambavyo vinatumia umeme na sola mashine 10 ambavyo vinauwezo wa kutotoresha kuku zaidi ya 200 katika ofisi ya UWT ili kupunguza michango kwa viongozi wanapokuwana mahitaji mbalimbali.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Anold Makombe amewaomba viongozi wote wa UWT wilaya ya Shinyanga amewaomba pale chama cha mapinduzi kitakapoteuwa wagombea wasikasilike ambao watakuwa hawajateuliwa kwani hawataweza kuteuliwa wote hivyo viongozi wasinung"unike kwani atakayechaguliwa ndiyo atakayepeperusha bendera ya CCM.

Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Getrude Mboyi amewashukuru wanawake kujitokeza kwa ajili ya kupata elimu ya maadili ya uongozi, hivyo anaamini wataenda kuifanyia kazi katika nyakati hizi za uchaguzi hawataenfa kuchagua viongozi ambao hawana maadili, wataleta viongozi bora ambao watawawakilisha na kutatua kero mbalimbali za jamii kwa wakati 
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza na viongozi wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza na viongozi wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza kwenye kongamano hilo
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza kwenye kongamano hilo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Anold Makombe akizungumza kwenye kongamano hilo
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha akizungumza kwenye kongamano hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza kwenye kongamano la UWT wilaya
Mwenyekiti wa Chsma cha mapiduzi CCM Annold Makombe akiwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo
Katibu muenezi wa wilaya ya Shinyanga Said Bwanga akizungumza kwenye kongamano la UWT wilaya
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha akitoa maada ya maadili ya kiongozi
Takelove Ayo kutoka Polisi Dawati la jinsia, .akitoa mada ya ukatili katika kongamano 
Afisa kutoka Takukuru akitoa mada ya rushwa katika kongamano la UWT
Mjumbe wa baraza la UWT mkoa wa Shinyanga Christina Gule akizungumza kwenye kongamano hilo
Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kongamano hilo
Viongozi kutoka kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kongamano hilo



Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo


Kazi ikiendelea


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464