MBUNGE WA JIMBO LA SOLWA AHMED SALUM ACHUKUA FOMU KUTETEA KITI CHAKE KWA AWAMU NYINGINE
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum,amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa ili kutetea tena kiti chake.
Amechukua Fomu hiyo leo Juni 28,2025 katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Ahmed amekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa tangu mwaka 2005.