Mtia nia wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Siha Mkoa wa Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Kennedy Mmari ameahidi kuifanya Siha kuwa kitovu cha mapinduzi ya kiuchumi na kiteknolojia huku akiahidi kudumisha Amani, Utulivu na Mshikamano pindi atakapopewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jumbo hilo. Akielezea nia yake ya kugombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Mmari amesema kuwa wakati wa Siha mpya ni sasa.
“Ninaamini katika teknolojia kwa maendeleo. Tutaanzisha kituo cha ubunifu kwa vijana, kuwezesha biashara mtandao na kushinikiza huduma za serikali kufanyika mtandaoni,” alisema Mmari.
Mbali na hilo, Mmari anasisitiza kuwezesha vijana na wanawake katika uchumi shirikishi:
“Tutavutiwa na uwekezaji unaoongeza thamani ya bidhaa zetu kama mazao, maziwa, nyama, ngozi na utalii. Lengo ni kuongeza ajira na kipato cha wananchi.”
Katika Ilani yake ya 2025–2030, ameainisha mipango kabambe ya kuimarisha elimu, kilimo, miundombinu, pamoja na TEHAMA kuanzia na shule zote za umma katika wilaya ya Siha. “Tupo kwenye nyakati za sayansi na teknolojia. Watoto wetu hawapaswi kuhitimu darasa la saba au sekondari ndiyo wakaanze kushangaa teknolojia. Watajifunza kuanzia shuleni”, amesema.