` HECHE:UCHAGUZI USOGEZWE MBELE KUPISHA MABADILIKO

HECHE:UCHAGUZI USOGEZWE MBELE KUPISHA MABADILIKO


MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Heche amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anasogeza uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais mbele ili kupisha marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Heche amesema hayo leo mkoani Morogoro wakati CHADEMA ilipofanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi K,ndege Manispaa ya Morogoro. Anasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina maeneo mengi ambayo yanaketa mkanganyiko ambazo zikifqhyiwa marekebisho nchi itapata viongozi sahihi watakaosaidia wananchi kuondokana na umaskini waliokuwa nao licha ya kwamba nchi yao ni tajiri.

Anasema pamoja na ukubwa wa Tanzania lakini nchi ina kila sababu ya wananchi wake kuitwa tajiri kutokana na mali zilizopo ikiwemo madini ya aina mbalimbali, makaa ya mawe, chuma na mchanga wa kusafishia ambavyo havisimamiwi wala kutumiwa vyema kutokana na usimamizi mbovu uliopo.

 Anasema CHADEMA ikipata nafasi ya kuongoza nchi baada ya katiba kurekebishwa mzee wa miaka 60 anapata bima ya maisha huku kukiwa na bima ya afya kwa wote.

SOMA ZAIDI Chanzo Nipashe

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464