Barrick yawekeza Dola Bil 4.24 kwenye shughuli za Uchimbaji madini Nchini
Na Edwin Soko
Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya Barrick imewekeza kiasi cha Dola billion 4.24 Nchini tangia ilipoanza shughuli zake Nchini 2019 .
Hayo yamebainishwa na Meneja Mkazi wa Barrick Nchini Daktari Melkiory Ngido alipokuwa anaongea na wahariri wa Vyombo vya habari kwenye makao Makuu ya Barrick Jijini Dar es salaam.
Doktari Ngido aliongeza kuwa Dola Bil 4.24 ni jumla ya mchango wa kiuchumi yangu Barrick ilipochukua jukumu la uendeshaji wa migodi Nchini Mwaka 2019.
" Hivyo napenda mtambue kuwa Barrick imekuwa mstari wa mbele kwenye kujivunia uwekezaji huo Kwa kuwa unaimarisha uchumi wa Nchi yetu" Alisema Daktari Ngido.
Naye Neema Ndosi, Afisa Mahusiano wa Barrick kwenye wasilisho lake la mafanikio ya Barrick alieleza mchanganuo wa Dola Billioni 4.24 kama.ifuatavyo, wachimbaji wazawa Dola bilioni 2.3 sawa na 55%, Kodi , mirabaha, tozo Dola bilioni 1.37 sawa na 32%, Mshahara Dola Milioni 397 sawa na 9% na gawio Dola Milioni 53 sawa na 4%.
Ndosi aliongeza kuwa uwekezaji Barrick imeendelea kuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa uchumi kupitia kodi zinazolipwa , ajira, miradi ya jamii na mgao kwa Kwa wanahisa wa Twiga.
Ndosi alibainisha kuwa, Dola bilioni 4.24 ziliwekezwa Nchini huku dola bilioni 1.5 (Tshs trilioni 3.6)zililipwa Kwa Serikali. 83% ya jumla ya matumizi yalikuwa ya ndani , huku 75% ikienda Kwa Kampuni za wazawa.
Kampuni ya Barrick pia imeendelea kufanya shughuli za kimaendeleo na kuimarisha hali ya maisha Nchini.
Kwa Mwaka 2024 Barrick ilitekeleza miradi kwenye kuboresha miundombinu ya afya, ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa maabara na ujenzi wa maktaba na jumla ya miradi 72 imekamikika kwenye sekta ya elimu.
Vile vile kwenye sekta ya miundo mbinu ya barabara, Barrick imejenga barabara ya kiwango Cha lami toka kakola hadi kahama yenye urefu wa kilomita 73 na kuboresha barabara ya German kwa kiwango Cha changarawe iliyopo Mara.
Meneja Mkazi wa Barrick Nchini Daktari Melkiory Ngido akizungumza.
Neema Ndosi, Afisa Mahusiano wa Barrick akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464