Na Marco Maduhu,SHINYANGA
NAIBU Waziri Kivuli,Habari,Mawasiliano na TEHAMA Emmanuel Ntobi, kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo,amechukua Fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama hicho.
Amechukua Fomu hiyo leo Juni 30,2025 katika Ofisi za ACT-Wazalendo Jimbo la Shinyanga Mjini,na kukabidhiwa na Fomu na Katibu wa Jimbo hilo Justa Denis.
Ntobi akizungumza mara baada ya kuchukua Fomu hiyo,amesema akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,atawatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo,pamoja na kutatua changamoto zao zote ambazo zinawakabili.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464