
Fedha zako haziwezi kuisha kwa urahisi ukifanya hili moja tu!
Unajua hakuna jambo linachosha na kuumiza kama kupata fedha, tena fedha nyingi lakini zinakuwa zinaisha bila kuona zimefanya kazi gani hasa, yaani fedha zinakuwa kama zinapita njia kwako tu. Inaumiza sana.

Ndivyo ilivyokuwa na kwangu pia, nilikuwa nafanya kazi na kupokea mshahara kila mwisho wa mwezi, lakini ukiangalia maisha yalivyo, hayana tofauti sana na mtu asiye na kazi!.