
Duh! wezi wajikuta wakipeleka gari la wizi kituo cha Polisi
Visa vya wizi wa magari vimekuwa vikiripotiwa kwa wingi katika maeneo mbalimbali humu nchini Kenya, kila wiki ningeweza kusikia habari kwenye chombo cha habari kisa kimoja au viwili vikiripotiwa kuhusu wizi wa gari, jambo ambalo sikuchukulia kwa uziri kwani nilidhani ni uongo tu.

Ni hivi majuzi ambapo niliweza kukumbana na wizi huo moja kwa moja baada ya gari laungu aina ya Harrier kuibwa katikati mwa jiji la Nairobi.