` WAGONJWA 194 WA MACHO WAMEPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

WAGONJWA 194 WA MACHO WAMEPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA


Wagonjwa 194 wa Macho Wamepatiwa Huduma za Kibingwa Hospitali ya Rufaa Shinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Wagonjwa zaidi ya 194 wa macho wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ya kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Taarifa hiyo imetolewa leo, Juni 6, 2025, na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Luzila John, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kambi ya utoaji wa huduma za kibingwa za macho.

Dkt. Luzila amesema kambi hiyo ilianza rasmi Juni 2, 2025, sambamba na uzinduzi wa huduma za kibingwa za macho katika hospitali hiyo.
“Kambi hii iliyoanza Juni 2 na kuhitimishwa leo Juni 6, tayari tumewahudumia wagonjwa wa macho zaidi ya 194 kwa kuwafanyia uchunguzi na kuwapatia matibabu,” amesema Dkt. Luzila.

Ameongeza kuwa baada ya kuhitimishwa kwa kambi hiyo, huduma hizo za kibingwa zitaendelea kutolewa kama sehemu ya huduma za kawaida na kwamba itakuwa ikitolewa mara mbili kwa wiki.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Macho, Dkt. Paul Kabuche, amewahimiza wananchi wa Shinyanga na mikoa jirani kufika hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya macho mapema, ili kuepusha athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kupata huduma.

Baadhi ya wagonjwa waliopatiwa huduma, akiwemo John Myola, wameishukuru serikali kwa kununua vifaa tiba na kuanzisha huduma hizo za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Shinyanga, ambapo wamesema hatua hiyo imewaepusha na gharama kubwa za kusafiri kwenda kupata huduma katika hospitali za Bugando na Muhimbili.

TAZAMA PICHA👇👇
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk.John Luzila akizungumza na waandishi wa habari
Daktari Bingwa wa Macho Dk.Joseph Kimaro akifanya uchunguzi wa macho
Daktari Bingwa wa Macho Dk.Paul Kabuche akifanya uchunguzi wa macho.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464