

Afisa wa ofisi ya wakala wa vipimo mkoa wa Shinyanga, Leo Patrick akitoa elimu katika kituo cha uzaji wa mafuta kwa vyombo vya usafiri juu ya umuhimu wa kutambua vipimo katika kuadhimisha siku ya vipimo duniani.
Na Kareny Masasy,
Shinyanga
WAKALA wa Vipimo
mkoa wa Shinyanga (WMA) umetoa elimu kwa baadhi ya waendesha bodaboda kwaajili ya kuthibiti Vipimo kwenye vituo vya
utolea huduma ya mafuta ili kujua hali halisi ya Vipimo wanavyovipata kama ni
sahihi.
Hayo
yamesemwa leo mei 20,2025 na Ofisa Vipimo, Leo Patrick
katika kuadhimisha siku ya vipimo duniani iliyoendana na utowaji wa elimu
na namna ya kutambuzi wa pampu yenye stika ya Wakala ya Vipimo iliyothibitishwa kwa matumizi halali ya utoaji
huduma na yenye kipimo halali.
Patrick amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni vipimo kwa Watu wote na Muda wote ikiwa
utoaji wa elimu hii lengo lake ni kubaini
pampu hizo kama zinatumika kwa kuendana na uhalisi wa Vipimo kama
inavyohitajika.
“Elimu leo
tumeitoa ili kuweza kuthibiti wimbi la wizi kwa watumiaji kwani dhima ya Wakala
wa Vipimo ni kuhakikisha mlaji au mtumiaji anakuwa kwenye hali ya Usalama,afya,kibiashara na Mazingira” amesema Patrick.
Patrick
amesema utoaji wa elimu kwenye vituo vya mafuta
ni moja ya eneo linalohusika na Wakala wa Vipimo kwa kuthibitisha kuwa Vipimo
ni sahihi ikiwa maeneo mengi wamekuwa
wakihusika katika kutoa elimu na kuthibiti kupunja walaji.
Ofisa Vipimo
Baraka Mbizo amesema leo ni siku ya vipimo
duniani na wametembelea kituo cha mafuta na kuna stika iliyopo
kwenye mashine inaonyesha ilikaguliwa lini
na mwisho wa matumizi ya pampu ni lini.
Mbizo
amesema muda wowote wamekuwa wakifanya
ukaguzi wa kushtukiza na wamekuwa
wakitoa elimu mara kwa mara na kuhakikisha pampu inakuwa inaanzia namba sifuri bila kuingiliana na mteja mwingine.
Mbizo
amesema pindi wakipata malalamiko kuwa
kituo fulani kinafanya udanganyifu na
uchunguzi ukafanyika na kubainika kuwa
kweli hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za Wakala wa Vipimo za mwaka 2002
kwa kutozwa faini .
Mbizo
amesema faini hizo zinazotozwa kwa mujibu wa sheria pindi
mmiliki akikutwa na makosa ambapo
itatozwa shilingi milioni 3 hadi tano au
kifungo cha miaka
mitatu kwenda jela.
Mwenyekiti wa kituo cha bodaboda mtaa wa ushirika,Frank Mahende alipongeza wakala wa vipimo kwa
elimu waliyoitoa kujua stika iliyowekwa
ina umuhimu wa kujua uhalali wa vipimo kwenye
mafuta wanaoupata kutokana na safari
wanazozunguka.
Mwendesha
bodaboda Hamis Mshandete mkazi wa ushirika manispaa ya Shinyanga amesema Wakala wa Vipimo wametoa elimu na amejifunza namna ya uwepo wa stika zilizo kwenye mashine ili kuweza kupata mafuta kupitia Vipimo halali.




Muuzaji wa sheli,maafisa wa ofisi ya vipimo na madereva boda boda wakifatilia elimu ya vipimo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464