Na Suzy Butondo, Shinyanga
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Habiba Musimu amewashauri viongozi wote wa UWT CCM wahakikishe wanawahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu, ili waweze kupiga kura ya kumchagua diwani, mbunge na Rais.
Licha ya kuhamasisha watu wajitokeze kujiandikisha daftari la kudumu pia amewashauri wanawake wajitokeze kugombea udiwani na ubunge, kwani inawezekana mwanamke kuwa kiongozi na kuweza kuongoza vizuri
Hayo ameyasema leo wakati akitoa maelekezo kwa viongozi wa UWT na chama katika kata ya Ndembezi na kata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga mkoani hapa.
"Uchaguzi mkuu wa kuwachagua diwani mbunge na Rais umekaribia hivyo niwaombe viongozi wote muwahamasishe wananchi wote waende kujiandikisha, na wale ambao bado hawajajisajili kwa ajili ya kupata kadi za chama za kielectroniki waende wakajiandikishe ili wapate kadi hizo, lakini pia kuna watu ambao kadi zao zimesha toka waende wakachukue kwenye ofisi zao,"amesema Musimu.
Zoezi la kuhamsisha limefanyika wilaya yote ya Shinyanga mjini ambapo viongozi wameahidi kuhamasisha wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha wakajiandikishe, ili waweze kupata kadi za mpiga kura, ikiwa ni pamoja na wanachama ambao hawajapata kadi za kielectroniki wakajisajili ili waweze kupata kadi hizo.



























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464