` REDESO NA CARE INTERNATIONAL WAINUA WAKULIMA KISHAPU KUPITIA UFUGAJI KUKU KISASA

REDESO NA CARE INTERNATIONAL WAINUA WAKULIMA KISHAPU KUPITIA UFUGAJI KUKU KISASA

  

Meneja miradi Care International Wilfred Makombe akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Afisa mifugo Kata ya Kiloleli Damla A. Damla akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Meneja miradi Redeso Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Charles Buregeya akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Kalekwa Mtoni akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Afisa wa Redeso Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Erica Karuta akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Diwani wa viti malum Kata ya Ukenyenge Mhe.Josephine Malima akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.
Katibu wa kikundi cha Muungano Kijiji cha Busongo Kata ya Mwamashele Suzan Ezekeil akizungumza Mei 28,2025 katika ziara ya kuwajengea uwezo wakulima wanafunzi jinsi ya kufuga kuku chotara kwa njia ya kisasa na kilimo cha bustani katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko tabia nchi unaotekelezwa na Redeso kwa kuwezeshwa na Care International.



Na Sumai Salum -  Kishapu

Katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Shirika lisilo la kiserikali REDESO kwa kushirikiana na CARE INTERNATIONAL, limeendeleza jitihada za kuwawezesha wakulima wadogo kwa kuwajengea uwezo katika mnyororo wa thamani wa zao la mkonge na ufugaji wa kisasa wa kuku.

Akizungumza Mei 28,2025 Meneja miradi kutoka Redeso Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Charles Bulegeya amesema kupitia mafunzo hayo kwa wakulima wanafunzi wanafundishwa mbinu bora za kufuga kuku chotara walioboreshwa wenye uwezo wa kustahimili magonjwa, kukua haraka na kuongeza kipato kisha wakafundishe kundi kubwa kwenye maeneo yao.

“Tunatoa elimu na kisha kuwawezesha kwa mitaji midogo ili waweze kuanza ufugaji kwa tija na kwa kutumia maarifa ya kisasa,” amesema Buregeya.

Mafunzo haya yameambatana na ziara ya wakulima kutembelea miradi ya wafugaji wenzao katika vijiji vya Isoso na Negezi, ambapo wamejifunza kwa vitendo, kubadilishana uzoefu, na kuhamasika kwa mafanikio ya wenzao ili wakawe chachu ya mabadiliko yenye kuzaa matunda kwenye maeneo yao.

Afisa mifugo wa Kata ya Kiloleli, Damla A. Damla, ametoa elimu kuhusu madhara ya kuchanganya kuku na bata katika eneo moja, akisisitiza kuwa bata hubeba vimelea visivyowaathiri wao lakini vinavyowaathiri kuku vibaya.

“Mfugaji atapata hasara kwa kutibu mara kwa mara, kuku wanaweza kufa, na chakula kinapotea kutokana na vyombo kuwekwa chini,” amesema Damla.

Diwani wa Viti Maalum Kata ya Ukenyenge, Mhe. Josephine Malima, amepongeza Redeso na Care International kwa uzalendo na uwezeshaji wa wananchi kupitia elimu ya kilimo na ufugaji wa kisasa.

Naye Mratibu wa mradi kutoka Care International, Wilfred Makomba amewatia moyo wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa na uthubutu wa kutekeleza mradi huu kwa bidii.

Baadhi ya wakulima na wanufaika akiwemo Suzan Ezekiel (Busongo), Rahel Charles (Mihama), na Reuben Nestory (Negezi) wameeleza mafanikio yao na shukrani kwa mafunzo waliyopewa.

“Tuliona ufugaji kuku ni wa kawaida, lakini sasa tumejifunza, tunapata kipato cha kusomesha watoto na kula vizuri. Tunajivunia kusema, Kuku ni Mfalme!” amesema Suzan, Katibu wa Kikundi cha Muungano Busongo.

Mradi huu unatekelezwa katika vijiji 10 vya Wilaya ya Kishapu: Shagihilu, Mihama, Busongo, Negezi, Uchunga, Kakola, Lubaga, Bubinza, Isoso na Unyanyembe, kwa ushirikiano wa karibu na maafisa mifugo wa Kata na Wilaya.

Kupitia jitihada hizi, Redeso na Care International wamekuwa nguzo ya mabadiliko ya kweli kwa wakulima wa Kishapu Kwa elimu, mitaji, na ufuatiliaji wa karibu, wakulima hawa wanabadilisha maisha yao na familia zao kwa kutumia rasilimali za asili na maarifa ya kisasa.
Jengo la Mradi wa kuku kikundi cha Jitolee B kilichoko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464