` AMREF,SERIKALI WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANANCHI WA ITILIMA WILAYANI KISHAPU

AMREF,SERIKALI WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANANCHI WA ITILIMA WILAYANI KISHAPU

AMREF,SERIKALI WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANANCHI WA ITILIMA WILAYANI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU

SHIRIKA la Kimataifa la Amref Health Africa, kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, limetoa elimu ya afya ya uzazi kwa wananchi wa Itilima Wilayani Kishapu.
Elimu hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya uhamasishaji wa afya ya uzazi. Tukio hilo liliambatana na huduma za upimaji wa afya kwa wananchi pamoja na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na mashindano ya kuvuta kamba.

Mwakilishi wa Amref Josiah Otege, amesema shirika hilo linashirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi kupitia mradi unaoitwa “Thamini Uzazi Salama”, unaotekelezwa katika kata saba za Wilaya ya Kishapu, na katika halmashauri nyingine ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
“Lengo la mradi huu”thamini uzazi salama” ni kuboresha afya ya uzazi ili kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi,”amesema Otege.

Naye Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma mkoani Shinyanga Moses Mwita,amesema kupitia mradi huo kwamba wanataka Mama abebe ujauzito na kujifungua salama,huku akiwasihi wanawake pale wanaposhika ujauzito wanapaswa kuhudhuria kwa mahudhurio yote nane, na waende wakiwa na wenza wao.
Aidha, amewasisitiza wanaume kwamba wawe wanawasindikiza wake zao kwenda Kliniki, ili wakapate kwa pamoja elimu ya afya ya uzazi pamoja na uzazi wa mpango na hata kumsaidia Mama katika ujauzito wake pamoja na matunzo kwa kuzingatia ushauri wa Wataalamu wa Afya na kujifungua salama.

Nao baadhi ya wanawake akiwemo Maria Charles, wamesema elimu hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao na itawasaidia kufuata taratibu sahihi za kiafya tangu mimba kutungwa hadi kujifungua.

Kwa upande wa baadhi ya wanaume akiwamo Ibrahimu Mhenga, wamesema elimu waliyoipata imewasaidia kubadilika, na sasa wako tayari kushiriki kikamilifu kwa kuwapeleka wake zao kliniki na kuwahudumia wakati wa ujauzito.

TAZAMA PICHA 👇👇
Mwakilishi wa Shirika la Amref Josiah Otege akizungumza kwenye utoaji wa elimu ya Afya ya uzazi.
Mratibu wa Elimu Afya kwa Umma wilaya ya Kishapu Mwajuma Abeid akizungumza.
Mratibu wa Elimu Afya kwa Umma wilaya ya Kishapu Mwajuma Abeid akizungumza.
Mtendaji wa Kata ya Itilima Masembe Mazozo akizungumza.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga Moses Mwita, akitoa elimu ya Afya ya uzazi kwa wananchi wa Itilima wilayani Kishapu.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga Moses Mwita, akitoa elimu ya Afya ya uzazi kwa wananchi wa Itilima wilayani Kishapu.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga Moses Mwita, akitoa elimu ya Afya ya uzazi kwa wananchi wa Itilima wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Itilima wilayani Kishapu Joseph Kulwa akizungumza.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464