
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao
Suzy Butondo Shinyanga
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewataka wazazi na walezi kuacha kujiweka bize na marejesho badala yake wawalinde watoto wao wa kike na wakiume ili wasifanyiwe ukatili na watu wenye nia mbaya..
Licha ya kuwalinda watoto, pia wanaume wametakiwa kuacha ukatili wa kulala na bukta na wanawake kulala na madela kwa kusababishwa na vikoba vingi kwa madai hawajisikii kufanya tendo la ndoa, kufanya hivyo ni kufanyiana ukatili.
Watoto wao wenye umri mdogo wasiwe tegemezi wa kuwalipia marejesho yao, kwani kufanya hivyo ni kama kumuuza mtoto ili mzazi utimize mahitaji yako, hali ambayo inaweza kumsababishia mtoto kupata mimba za utotoni au magonjwa.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na Viongozi wa UWT katika kata za Lubaga, Ndala na Shinyanga mjini wakati akiendelea na ziara yake ya kamati ya utekelezaji ya UWT wilaya ya Shinyanga mjini, ambapo amesema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaona watoto wao wanarudi na fedha, nguo na vitu mbalimbali na kufurahia kuwa wanasaidiwa,bila kuwauliza fedha hizo wametoa wapi.
"Niwaombe wanawake wenzangu wale tunaoruhusu watoto wetu kufanya matendo kama haya tuache mara moja, kwani kufanya hivyo tunawaharibu sisi wenyewe watoto wetu, baadae watakuja kutushinda na kusababisha mimba za utotoni na watoto wa kiume kuwa mashoga, wakati mwingine magonjwa kabisa, niwaombe tuwalee katika maadili mema ya kidini ili baadae wakiwa wakubwa tufaidi matunda yao"amesema Nhamanilo.
Pia aliwataka waache kuwatuma watoto usiku madukani, kama ni usiku anatakiwa kwenda mtu mzima si mtoto, na pia wawakague mara kwa mara wanapowaogesha kwa sababu watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili bila wazazi kujua,lakini wakiwakagua na kukuta wamefanyiwa ukatili wa kulawitiwa au kubakwa wanaweza kuwawahisha kwenye matibabu na kuweza kudhibiti wasiendelee na tabia hiyo.
Pia Nhamanilo akiwa katika kata hizo alisisitiza viongozi wasiendeleze makundi "Naahidi kwamba nitasema kweli daima ili tusikiuwe chama chetu, niwaombe kabisa tukemee makundi hayo,ili tuweze kupata ushindi mkubwa tuweni wamoja, na tujitathimini, usiombe hela kwa wagombea kwa kumchafua mtu,kwa kupeleka uongo uongo tuendelee kuyakemee makundi ndani ya jumuiya yetu ya UWT".
"Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Juliana Buzuluga amesema watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili na ndugu unaweza kukuta mjomba au ndugu wengine wa karibu hivyo tusiwaamini sana mpaka tukawalaza kwenye chumba kimoja na wageni wanaokuja majumbani kwetu ambao hatuwajui hata tabia zao,"amesema Buzuluga.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mariam Kajala amewashauri wanawake wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuomba nafasi za udiwani na ubunge, na kuwataka wapendane washirikiane katika kufanya kazi za jumuiya na chama.
Diwani wa kata ya Ndala ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Zamda Shaban amesema Rais Samia Suluhu ameleta fedha nyingi sana katika kata hiyo kwa ajiki ya kufanya miradi mbalimbali ambayo haikuwepo, z
katika sekta ya elimu, miundombinu ya barabara, afya,na umeme,hivyo wameshirikiana na mbunge Patrobas Katambi katika kuisimamia miradi hiyo.
Katibu wa Umoja wa wanawake wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi amewataka viongozi wote kuanzia ngazi za matawi wawe wanafanya vikao vyao vya kikanuni, ili wajumbe waweze kujua nafasi zao na wanachama kuwa hai, pia wahamasishe watu waendelee kujisajili ili waweze kupata kadi za kielektroniki.
"Niwaombe viongozi wangu wite kuanzia kwenye matawi endeleeni kulipa ada, kwani ada ndiyo zinakuonyesha wewe kwmba ni mwanachama hai, hivyo kola mmoja akalipie pia hamasidheni wamawake waweze kujiunga na UWU maana kuna wanawake wapo kwenye chama lakini UWT hawapo"amesema Mboyi.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo na Chama
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Salome Abuolo akizungumza
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mariam Kajala akizungumza

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao
Diwani wa kata yaNdala Zamda Shaban akizungumza na viongozi
Mwenyekiti naviongozi wake wakiendelea na burudani katika kata yaNdala