` MATESO MAGUMU YA UGONJWA WA NGOZI KWA MIAKA 22 KWA FRANK MAHEGA MAKANDILA

MATESO MAGUMU YA UGONJWA WA NGOZI KWA MIAKA 22 KWA FRANK MAHEGA MAKANDILA

 



MATESO MAGUMU YA UGONJWA WA NGOZI KWA MIAKA 22 KWA FRANK MAHEGA MAKANDILA


 Maswa, Simiyu – Mei 20, 2025

Frank Mahega Makandila (22), mkazi wa kijiji cha Mwakidiga, kata ya Lalago – Maswa, amekuwa akiishi kwenye mateso makubwa tangu kuzaliwa kutokana na ugonjwa wa ngozi wa nadra unaomsababishia kuota nyama zenye magamba na kuwashwa kupita kiasi kila siku.

Akizungumza na Shinyanga Press Club Blog, Frank alieleza kuwa kwa zaidi ya miongo miwili, maisha yake yamekuwa ya maumivu yasiyoisha huku familia yake ikihaha kutafuta tiba kwenye vituo mbalimbali vya afya nchini bila mafanikio. Hali hiyo imesababisha familia yake kufilisika kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwa matibabu yasiyokuwa na suluhisho la kudumu.

“Nimesumbuka tangu utotoni. Familia yangu imehangaika kwa miaka mingi bila mafanikio. Naomba Watanzania wenye moyo wa huruma wanisaidie niweze kupata matibabu kwenye hospitali kubwa hapa nchini,” alisema Frank kwa uchungu.

Kwa sasa, Frank amepatiwa kibali rasmi na serikali ya kijiji na wilaya ya Maswa kuomba msaada kutoka kwa watu wenye mapenzi mema ili aweze kupata tiba anayohitaji.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwakidiga, Daniel Josephat, alitoa barua rasmi ya utambulisho, ambayo imethibitishwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa.

Kwa yeyote mwenye nia ya kumsaidia Frank, msaada wa fedha unaweza kutumwa kupitia namba ya simu:

📞 0794-884713 (Frank Mahega Makandila)

Frank ana matumaini kuwa kwa msaada wa Watanzania na watu wenye huruma, ataweza kupata afueni na kuishi maisha ya kawaida kama vijana wenzake.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464