` KAMATI YA UTEKELEZAJI YAHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO: KWA KUWATAKA VIONGOZI KUACHA KUWAPIMA KWA FEDHA ZAO BALI WAWAPIME KWA UWEZO WAO

KAMATI YA UTEKELEZAJI YAHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO: KWA KUWATAKA VIONGOZI KUACHA KUWAPIMA KWA FEDHA ZAO BALI WAWAPIME KWA UWEZO WAO


Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga akisalimia na viongozi mbalimbali UWT pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM

Suzy Butondo, Shinyanga

Kamati ya utekelezaji ya UWT wilaya ya Shinyanga mjini ikiongozwa na mwenyekiti wake Rehema Nhamanilo,  leo imehitimisha ziara yake kwa kishindo kikubwa katika kata za Kolandoto, Chamaguha na Kitangili.huku ikiwataka viongozi kuacha kuwapima viongozi kwa fedha zao badala yake wawapime kwa uwezo wa kuongoza na maendeleo waliyoyafanya.

Akizungumza na viongozi wa kata hizo mwenyekiti Nhamanilo  amesema baadhi ya viongozi wa kata wamekuwa wakiwabeza viongozi wao kwamba hawajafanya chochote kwenye majimbo yao na kuwasifia wale wanaowania kugombea kwenye nafasi hizo ili wapewe fedha

"Acheni kuwapima watu kwa fedha yao wapimeni kwa uwezo wa maendeleo wanayoyafanya, mnaweza mkachagua mtu mwenye fedha akashindwa kuwawakilisha vizuri kwa sababu mliangalia fedha hamkuangalia uwezo wake wa kufanya kazi jisimamieni mkatae kuyumbishwa kiongozi bora anatakiwa kusimama na kiongozi aliyeko madarakani mkibebelea wengine vichwa vitawauma jueni kwama mpaliliaji hana shamba, "amesema Nhamanilo.

Tukumbuke tunawatoto tunadomesha ambao tunategemea baadae wanakuja kuwa wabunge,mawaziri jetukiendekeza fedha na watoto wetu wakihitaji kuwa viongozi wakajikuta hawana fedha llakini uwezo wa kuongoza wanao itakuwaje,tuacheni kuendekeza fedha, tuwathamini viongozi ambao wanatuwakilisha vyema, tukichagua wenye fedha baadae watatutelekeza na kutuacha wakiwa huku wao wakiendelea kujinufaisha wenyewe,,"ameongeza Nhamanilo.

Aidha amesema kuna baadhi ya watu kazi yao kutafuta wagombea kwa kuwadanganya kwamba waje watawatafutia (Creem) ya watu, "sisi wote ni chama kimoja, tuheshimiane na tuheshimu viongozi walioko madarakani, Unapowagawa watu unaleta mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi, viongozi msiwagawe wanachama, niwaombe tuwe makini watu ambao wamekuwa wafanyabiashara wa wagombea, kama kuna mgombea anataka kuwanufaisha watu awanufaishe wote asiwagawe wanachama."

"Pia niendelee kuwasihi wanawake wenzangu muache kuwafanyia ukatili wenza wenu kwa kuwapiga vipepsi kwa madai kwamba wana strees ya kausha damu, wawape haki yao waume zao wanapohitaji haki yao ili kuwaepusha na michepuko isiyo ya lazima acheni kurudi nyumbani na stress zenu" amesisitiza na kuongeza .

"Wanaume wengi wamekuwa wakikimbilia michepuko kwa sababu ya kukosa haki yao ndani ya ndoa zao, hivyo wanakimbilia kwenye michepuko ili kutimiza haki yao,tubadilike wanawake tusiendelee kuwafanyia ukatili waume zetu ni wajibu wetu kuzituna familia zetu "amesema.

Mwenyekiti aliambatana na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ambao ni Juliana Buzuluga, Salome Abuolo, Nahima Masanja Mariam Kajala na katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi, ambao leo wamehitimisha ziara hiyo ambayo ilikuwa ya kuimalisha uhai wa UWT na chama CCM.
































































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464