` DC KISHAPU : WAUGUZI TUTUMIE MUDA WA KAZI KUWAHUDUMIA WAGONJWA KWA MOYO WOTE

DC KISHAPU : WAUGUZI TUTUMIE MUDA WA KAZI KUWAHUDUMIA WAGONJWA KWA MOYO WOTE

 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Wilayani Humo Mei 30,2025 yaliyofanyika ukumbu wa hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete- Picha na Sumai Salum
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akikabidhi zawadi kwa mzazi Elizabeth Mwandu kutoka kijiji cha Bulekea. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi (kushoto) akimpa pongezi Muuguzi Mkuu Wilaya hiyo DNO. Marium Ndahani kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani kiwilaya yaliyoadhimishwa Mei 30,2025 katika ukumbi wa hospitali ya Dr. Jakaya yenye kauli mbiu "Wauguzi nguvu ya mabadiliko Duniani"

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi, amewataka wauguzi na wakunga Wilayani humo kufanya kazi kwa mshikamano, upendo, kuheshimiana, kuheshimu muda wa kazi, na kuwathamini wateja wao, akisisitiza kuwa wananchi hao ndio sababu ya wao kuwepo katika nafasi hizo.

Mhe. Masindi ametoa wito huo leo Mei 30,2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mgeni rasmi.

Katika hotuba yake Mkuu huyo wa Wilaya amekemea vikali tabia ya baadhi ya wauguzi kutumia simu zao wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa, akisema hali hiyo huwavunja moyo wagonjwa na kuwafanya wajisikie kutopewa thamani.

“Tutumie muda wa kazi kuwahudumia wagonjwa kwa moyo wote. Simu zisizo na tija kazini ni kikwazo kwa utoaji huduma bora,” amesisitiza Mhe. Masindi.

Aidha, ameonya tabia ya wagonjwa wenye bima za afya kukosa dawa kwenye dirisha la dawa na kulazimika kununua dawa hizo kwenye maduka ya hospitali huku akiwataka wauguzi kujiepusha na vitendo vya dhuluma kwa akina mama wajawazito, akisema hayo ni kinyume na maadili, kanuni na sheria za serikali.

“Halmashauri iko macho na Wilaya yote na vitengo vyake viko macho hivyo Mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake bila kujari cheo na heshima yake aliyonayo”, amesema Mhe. Masindi.
Amewataka wauguzi kufanya vikao vya mara kwa mara ili kukumbushana kuhusu maadili na nidhamu kazini, akiongeza kuwa ni aibu kwa muuguzi kusimamishwa kazi au kufukuzwa kwa sababu ya uzembe au kupokea rushwa muendelee kudai haki zetu kwa njia halali, si kwa kuiba haki za wengine,” ameongeza.

Akiwahimiza wauguzi kutimiza majukumu yao kwa moyo wa huruma, Mhe. Masindi amesema: “Afya za wananchi zipo mikononi mwao wanapofanya kazi wakumbuke kiapo cha kazi yao, hasa katika kuokoa afya za kina mama na mtoto.”

Pia amewapongeza wauguzi kwa kazi kubwa wanayoifanya, akiwakumbusha kuwa wao ni watu wa kwanza kuwashika watoto wote wanaozaliwa duniani akitoa mfano wa injili amesema ilienezwa na watu12 tu wao ni zaidi yao wasikate tamaa kwa sababu ya uchache weo waendelee kufanya kazi kwa bidii na moyo wa kujitolea.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bw. Fadhiri Mvanga, amewapongeza wauguzi kwa moyo wa utu, uzalendo, upendo na uvumilivu waliouonyesha hasa wakati wa milipuko ya magonjwa kama kipindupindu amesema wauguzi hao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa jamii, licha ya hatari wanazokutana nazo kazini.
Diwani wa Kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson

Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson ametoa pongezi kwa wauguzi kwa kuadhimisha siku yao wakiwa kazini huku wakitoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali wakiwemo mama wajawazito, waliokwisha jifungua na watoto na ametoa wito kwa serikali kuanzisha chuo cha uuguzi katika Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ili kuongeza idadi ya wauguzi na kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Muuguzi Mkuu wa Wilaya (DNO), Bi. Mariam Ndahani, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa ataendelea kusimamia vema kada ya uuguzi ili ifanye kazi kwa weledi mkubwa sambamba na jitihada za serikali ya awamu ya sita kusikiliza na kutatua changamoto za wauguzi, ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao.

“Maadhimisho haya hufanyika kila Mei 12. Mwaka huu tumeadhimisha leo kwa ngazi ya Wilaya ili tukumbushane kuhusu kiapo na maadili ya kazi yetu ya uuguzi hii ni kazi ya baraka, tuendelee kuitumikia kwa moyo na wito wa kweli,” amesema DNO Ndahani.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo "Wauguzi nguvu ya mabadiliko duniani" yameambatana na maandamano huku wakitoa zawadi kwenye wodi mbalimbali na baadhi ya Wagonjwa waliopokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Wilayani Humo Mei 30,2025 yaliyofanyika ukumbu wa hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete- Picha zote na Sumai Salum
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Fadhiri Mvanga akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya waugudi kiWilaya Mei 30,2025 katika ukumbi wa hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete
Mkuu wa wauguzi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Dno.Mariam Ndahani akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Wilaya hiyo Mei 30,2025 yaliyofanyika ukumbi wa hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho kikwete yaliyoambatana na maandamano na utoaji zawadi kwa wagonjwa wa wodi zote huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi.
Baadhi ya wauguzi na wakunga wakifurahia maadhimisho ya siku yawakunga duniani Wilaya ya Kishapu Mkoani shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akikabidhi zawadi kwa Elizabeth Mwandu kutokea kijiji cha Bulekea.
Baadhi ya wauguzi na wakunga wakiingia hospitali ya Dr.Jakaya baada ya maandmano na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi Mei 30,2025
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464