Afisa habari Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Josephine Charles.
Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kimetambulisha mfumo mpya wa kutuma maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali za afya wanazofundisha chuoni hapo.
Mfumo huo ambao niwa ku Scan kupitia QR Code umetambulishwa kwa maaskari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga leo ambao walikuwa kwenye mazoezi ya utayari ili waweze kufikisha ujumbe kwa jamii inayowazunguka.
Mfumo wa QR Code utamuwezesha mtu kutuma maombi kwa wepesi na haraka ndani ya sekunde 30 tu tofauti na mfumo waliokuwa wanautumia hapo awali wa kutuma maombi kupitia tovuti ya chuo.
Mbali na kutambulisha mfumo huo, Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga pia kimetoa Elimu, kutangaza Fursa na kozi wanazofundisha chuoni hapo ili kuwahamasisha maaskari Polisi na jamii nzima kwa ujumla kujiunga na kujiendeleza katika fani za Afya.
Aidha kozi za afya wanazofundisha hapo ni pamoja na Clinical medicine, Nursing & midwifery, Physiotherapy, Pharmaceutical Sciences, Medical Laboratory na Radiology, pia kozi za Ufundi ni Computer na Laboratory assistant.
Kwa upande wa fursa chuo hicho pia kina kozi tatu zinazopewa mkopo na Serikali kwa ngazi ya Diploma ambazo ni RADIOLOGY, PHYSIOTHERAPY NA MEDICAL LABORATORY, hivyo jamii imeombwa kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ili kukabiliana na hali ya uchumi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464