` CCM KUZINDUA ILANI YA UCHAGUZI KWA KISHINDO JIJINI DODOMA

CCM KUZINDUA ILANI YA UCHAGUZI KWA KISHINDO JIJINI DODOMA

CCM KUZINDUA ILANI YA UCHAGUZI KWA KISHINDO JIJINI DODOMA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuzindua Ilani yake ya Uchaguzi itakayogusa moja kwa moja maslahi ya wananchi, katika Mkutano Maalum wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 29 hadi 30, mwaka huu jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa leo Mei 23,2025 na Katibu wa Nec Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makala wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Amesema ilani hiyo imeandaliwa kuwa kuzingatia mahitaji hali ya wananchi na kwamba ni ya matumaini makubwa kwa taifa, sababu walizingatia maoni na mapendekezo kutoka kwa wananchi wenyewe.
“Yajayo yanafurahisha,ilani ambayo tunakwenda kuizindua ni ilani ya wananchi,”amesema Makala.

Aidha, amesema katika Mkutano huo, wana wahidi wananchi, kwamba katika uchaguzi Mkuu,watawaletea wagombea safi wanaokubalika,pia uchaguzi utakuwa huru na haki,watafanya kampeni za kistaarabu bila ya kukejeli wagombea wa upinzani,na kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Pia,amewataka wananchi wa Shinyanga kwamba watunze vitambulisho vyao vya kupigia kura,sababu uchaguzi utakuwepo kwa mujibu wa katiba ya nchi, na siku hiyo ya uchaguzi washiriki kwa wingi pamoja na kuchagua viongozi wote wanaotokana na CCM sababu ndiyo wenye kuwaletea maendeleo.
Katika hatua nyingine, amesema kauli ya Chadema ya "No Reforms No Election" yani hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi, ni dalili za kushindwa,kwa kuogopa uchaguzi sababu mabadiliko ambayo wanayadai tayari yalishafanyiwa kazi chini ya utawala wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

"Ajenda ya Chadema siyo No Reforms No Election,bali wamechoka chama hiki kimekimbiwa na maelfu wa wanachama wao Chama kimesambaratika,”amesema Makala.
Ametaja mabadiliko ambayo yamefanyika ikiwamo kuundwa kwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambayo lilikuwa ni hitaji la Chadema, pia uchaguzi hautasimamiwa tena na Wakurugenzi wala hakuna tena kupita bila kupingwa bali kutakuwa na kupigiwa kura za ndiyo na hapana.

Aidha,amempongeza Rais Samia kwa kuletwa fedha za miradi ya maendeleo mkoani Shinyanga,na kuubadilisha mkoa huo, huku akionyesha kukerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanadai Mkoa huo hauna maendeleo na wananchi wake ni maskini, na kwamba kwenye mikutano hayo wakishamaliza huwachagisha fedha wananchi na kuhoji nani maskini wananchi au wao wanaochangisha fedha.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza katika Mkutano huo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni humo na kutekelezwa miradi ya maendeleo.

Mbunge wa Vitimaalum Christina Mnzava, amesema Mkoa wa Shinyanga hawana deni na Rais Samia sababu kila kijiji kimefikiwa na miradi ya maendeleo na kwamba ahadi yao kwao ni kumpatia kura nyingi za ushindi.

TAZAMA PICHA👇👇
Katibu wa Nec Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makala akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara mjini Shinyanga.
Katibu wa Nec Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Amosi Makala akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano huo pamoja kuwakaribisha Wanachama wa Chadema na Act-Wazalendo ambao wamehamia CCM, na kupolewa na Mwenezi Amosi Makala.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzamva akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shoinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464