` KATAMBI ATAJA MAFANIKIO YA MIAKA MINNE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO

KATAMBI ATAJA MAFANIKIO YA MIAKA MINNE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO

KATAMBI ATAJA MAFANIKIO YA MIAKA MINNE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), amesema jimbo hilo limepiga hatua kubwa za maendeleo ndani ya kipindi cha miaka minne.
Amebainisha hayo leo Mei 23,2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Town mjini Shinyanga, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na kuongozwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amosi Makalla.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan Jimbo la Shinyanga Mjini limepiga hatua kubwa kimaendeleo ambapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imekamilika na sasa inahudumia wananchi,vilevile Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga imekarabatiwa na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema katika sekta hiyo ya afya, zahanati tisa mpya zimejengwa pamoja na kituo cha afya cha Ihapa. Pia katika huduma hizo za afya kuna vifaa tiba vya kisasa pamoja na upatikanaji wa magari mengi ya wagonjwa ambulance.

Katika sekta ya miundombinu, Katambi amesema serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli wenye thamani ya Sh. bilioni 49, ambao kwa sasa uko katika hatua za mwisho na ndege tayari zimeanza kutua.

Aidha, amesema serikali inatarajia kujenga pia stendi mpya ya mabasi ya kisasa kwa gharama ya Sh. bilioni 19 ili kuimarisha huduma za usafiri, na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Shinyanga.

"Maendeleo yaliyopatikana katika jimbo hili ni makubwa kiasi kwamba kuyazungumzia yote kwa kina kunahitaji angalau siku mbili," amesema Katambi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amesema ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, mkoa huo umepokea zaidi ya Sh. trilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Katibu wa NEC, Itikadi,Uenezi na Mafunzo Amosi Makalla, amesema ameshuhudia mapinduzi makubwa ya maendeleo katika Jimbo la Shinyanga Mjini na mkoa kwa ujumla, akisisitiza kuwa Shinyanga ya sasa siyo ile ya zamani.
Makalla amewataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 wanawachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuendeleza kasi ya maendeleo iliyopo.

TAZAMA PICHA👇👇
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amosi Makalla akizungumza.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amosi Makalla akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza.
Mkutano ukiendelea.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464