WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI JIJINI MWANZA


WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI JIJINI MWANZA

Na Marco Maduhu,MWANZA

Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza na Shinyanga, wametembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika Jiji la Mwanza.

Ziara hiyo imefanyika leo Mei 2,2025 ambayo imeongozwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwahabarisha wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa vivuko vipya vitano, daraja la Busisi, pamoja na meli ya MV Mwanza ambayo kwa sasa imekamilika kwa asilimia 98.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Msigwa amesema miradi hiyo inalenga kuondoa changamoto za usafiri na usafirishaji, sambamba na kuchochea ukuzaji wa uchumi katika ukanda wa Ziwa Victoria na taifa kwa ujumla.

“Miradi hii ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita katika kuleta maendeleo ya kweli na ya haraka kwa wananchi,tunataka wananchi wote wajue kinachoendelea na wawe sehemu ya mafanikio haya,” amesema Msigwa.

Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea kesho mkoani Shinyanga, ambapo waandishi wataendelea kutembelea na kuripoti kuhusu utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali.








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464