KATAMBI ATIMIZA AHADI,ATOA MILIONI 2.6 KWA VIKUNDI 26 VYA MICHEZO YA JADI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,ametimiza ahadi yake kwa vikundi vya michezo ya jadi, kwa kutoa jumla ya sh.milioni 2.6 kama zawadi kwa washiriki wa mashindano hayo.
Fedha hizo zimekabidhiwa leo Mei 19,2025, na Katibu wa wake Samweli Jackson kwa niaba ya Mbunge Katambi, katika hafla fupi iliyofanyika Ofisi ya Mbunge.
Saweli akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo amesema kuwa Mbunge Katambi alitoa ahadi hiyo Mei 16, mwaka huu, wakati wa fainali ya michezo Jadi iliyofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage, akiahidi zawadi ya Sh. 100,000 kwa kila kikundi kilichoshiriki.
“Mbunge Katambi ndiyo mdhamini wa mashindano haya ya michezo ya Jadi,na alitoa zaidi ya sh. milioni 6, na kama sehemu ya kuthamini ushiriki wa vikundi vyote, aliahidi kuwapa zawadi ya sh. 100,000 kwa kila kikundi,leo ametimiza ahadi hiyo kwa vikundi 26,na nimekabidhi sh. milioni 2.6 ” amesema Samweli.
Amesema kuwa,Katambi ameahidi kuendelea kuunga mkono michezo hiyo ya jadi,kwa lengo la kuenzi na kudumisha mila na desturi za kitanzania.
Katibu wa Michezo ya Jadi Wilaya ya Shinyanga Mjini,Fabiani Francis, amempongeza Mbunge huyo pamoja na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zao za kufufua michezo hiyo ambayo ilikuwa imesahaulika kwa muda mrefu.
“Michezo ya Jadi ni muhimu katika jamii, sababu ni kielelezo cha Taifa na urithi wetu,”amesema Fabiani.
Naye Mwenyekiti wa Michezo ya Jadi Wilaya ya Shinyanga Mjini,Janeth Seseja, amemshukuru Katambi kwa moyo wake wa kujitolea na kusaidia kuendeleza michezo ya Jadi.
Baadhi ya wawakilishi wa vikundi vilivyopokea zawadi hizo, akiwemo Shoka Binkisu, wamemshukuru Mbunge Katambi kwa kuwa karibu na wananchi, na kuonyesha kuguswa na matukio ya kijamii, huku wakimpongeza kwa moyo wake wa kutoa.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akikabidhi fedha sh.milioni 2.6 kwa viongozi wa michezo ya Jadi kwa ajili ya kugawanywa kwa vikundi 26 vya michezo hiyo.
Mwenyekiti wa Michezo ya Jadi wilaya ya Shinyanga Mjini Janeth Seseja akizungumza.
Katibu wa Michezo ya Jadi wilaya ya Shinyanga Fabian Francis akizungumza.
Msanii wa Nyimbo za Asili Shokabin Kisu akizungumza.
Picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464