TANZANIA YAPANDA NA KUONGOZA AFRIKA YA MASHARIKI KWENYE KUHESHIMU UHURU WA HABARI


TANZANIA YAPANDA NA KUONGOZA AFRIKA YA MASHARIKI KWENYE KUHESHIMU UHURU WA HABARI

NIkiwa Mwandishi mkongwe na mtetezi wa haki ya kulinda uhuru wa habari, nimeiona na kuisoma taarifa ya kutathimini hali ya kuheshimu uhuru wa habari Duniani na kuona ni vyema niichambue kidogo ili iwe rahisi kwenye kujielewa. Tanzania) imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya kimataifa vya kuheshimu uhuru wa habari kwa mwaka 2025, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa la *Reporters Without Borders* (RSF).

Kwa mwaka 2025, Tanzania imeshika nafasi ya 95 kati ya nchi 180 duniani, ikilinganishwa na nafasi ya 97 mwaka 2024. Kupanda huko ni ishara ya hatua chanya zinazochukuliwa nchini katika kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari.

Kwa mafanikio haya, Tanzania imeongoza ukanda wa Afrika ya Mashariki katika kuheshimu uhuru wa habari. Nchi nyingine katika ukanda huo zimeorodheshwa kama ifuatavyo:

1.Sudan Kusini – Nafasi ya 109

2.Burundi – Nafasi ya 125

3.Kenya – Nafasi ya 127

4.Uganda – Nafasi ya 143

5.DR Congo – Nafasi ya 133

6.Rwanda – Nafasi ya 146

Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa Tanzania imepanda katika viashiria vitatu kati ya vitano vinavyotumika kupima uhuru wa habari, ambavyo ni:

1. Kiashiria cha Siasa: kutoka nafasi ya 94 (2024) hadi 87 (2025)

2. Kiashiria cha Uchumi: kutoka nafasi ya 108 (2024) hadi 87 (2025)

3. Kiashiria cha Sheria: kutoka nafasi ya 120 (2024) hadi 113 (2025)

Hata hivyo, Tanzania imeporomoka katika viashiria viwili:

1. Kiashiria cha Kijamii: kutoka nafasi ya 82 (2024) hadi 92 (2025)

2. Kiashiria cha Usalama: kutoka nafasi ya 98 (2024) hadi 107 (2025)

Takwimu hizo ni ishara njema Kwa waandishi wa habari wote Nchini Kwa kuwa unaleta matumaini Kwa vyombo vya habari Kwa kuimarika Kwa mazingira ya kazi Kwa waandishi wa habari Tanzania.

Pia kuimarika Kwa kuheshimu uhuru wa Vyombo vya habari kunaiweka Nchi katika jicho zuri la diplomasia ya kimataifa

Binafsi yangu nimekuwa mfuasi mkubwa sana wa kufuatilia uhuru wa habari Duniani, Kwa takwimu hizo niwape hongera waandishi wote wa habari, taasisi za kihabari, Serikali ya AWAMU ya sita na wadau wengine wote walioko kwenye mnyororo wa thamani wa kulinda uhuru wa habari Tanzania.

Tunaelekea kwenye maadhimisho ya uhuru wa Vyombo vya habari Tanzania Mei 03, 2025 tunanapaswa kufanya tafakuri zaidi ya namna ya kuongeza juhudi za kulinda uhuru wa habari Tanzania .

*Edwin Soko*

*Mwanahabati*
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464