Vyama vya Siasa vimetakiwa kulinda Uhuru wa Habari kipindi cha uchaguzi mkuu 2025
Na Marco Maduhu,ARUSHA
MKURUGENZI wa Jamii Africa, Maxence Mello, amevitaka vyama vya siasa kulinda uhuru wa habari na kuepuka kutoa vitisho kwa waandishi wa habari,hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 wa kuchagua madiwani, wabunge,na Rais.
Akizungumza leo, Aprili 28, 2025, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha, Mello amesema vyombo vya habari vinapaswa kufanya kazi zao kwa weledi ili kuuhabarisha umma kwa kina na kwa usahihi.
"Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, tunaomba vyama vya siasa vilinde uhuru wa habari na wasitoe vitisho wala matamko ya kuwatisha waandishi wa habari, ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi na kuuhabarisha umma kwa taarifa sahihi na za kina," amesema Mello.
Katika hatua nyingine,amewataka waandishi wa habari kuwa waangalifu na matumizi ya teknolojia ya akili bandia (AI) katika uandaaji wa maudhui yao, hasa wakati wa uchaguzi, ili kuhakikisha habari wanazotoa ni sahihi na haziathiri maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu 2025 inasema"Athari za Akili Bandia kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari na Tasnia ya Habari."
TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi wa Jamii Africa,Maxence Mello akizungumza.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko akichangia mada.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe Salome Kitomari akichangia mada.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464