Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba Ruhoro amesema nchi ya Tanzania inazalisha vyakula vya kutosha hadi watu kusaza na hivyo kuwaomba watanzania kupuuza watu wachache wanaohamashisha maandamano nchini hasa wale wanaotumia mitandao kufanya vikao Vya kichochezi kwani hakuna sababu za kufanya waandamane.
Mbunge huyo amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kumubuga Kata ya Nyamagoma Wilayani Ngara huku akisema kuwa mipango ya watu wanaohamasisha maandamano haitafanikiwa.
Aidha amesema kuwa watanzania wana Uhuru wa kutumia Ardhi kuzalisha vyakula tofauti na baadhi ya nchi ambapo Ardhi inamilikiwa na watu wachache na kufanya watu wengi kuteseka tofauti na hali ilivyo nchini Tanzania.
"Watanzania wanazalisha vyakula vya kutosha na kusaza hadi kuwauzia majirani zetu. Kwa namna hii watanzania hatuna sababu ya kuunga mkono watu wanaotaka kuleta vurugu ili kuwafanya watanzania walale njaa" ,amesema Mbunge huyo.
“Watanzania wana uhuru wa kutumia Mito, Maziwa na Bahari kwenye uvuvi jambo linalowafanya kujipatia mboga na kipato bila kusumbuliwa na mtu yeyote yapo Mataifa yenye Sheria ngumu na maeneo mengi Mito na maziwa yanasimamiwa na wawekezaji na hivyo kuwanyima fursa wananchi wa Kawaida tofauti na ilivyo hapa Tanzania”,amesema Mbunge Ruhoro.
Kuhusu ksekta ya Mifugo, amesema Watanzania tuna uhuru wa kutosha kufuga mifugo yao kama vile wanafuga kuku, Bata, Kondo, Mbuzi na Ng’ombe ikilinganishwa na baadhi ya Mataifa hairuhusiwi kufuga Bila kupewa kibali na idadi ya mifugo hasa Ng’ombe wasizidi watano tafauti na hali ilivyo Tanzania.
Ametoa mfano mwingine kuwa kuna nchi hasa zile zenye machafuko na migogoro ya mda mrefu uhuru wa kutembea umeminywa ukilinganisha na Tanzania ambapo Mtanzania akitaka kwenda kutembea hana kizuizi chochote kile ni yeye na nauli yake huku akikemea kikundi cha watu wachache wenye uchu wa madaraka ya kumpiga vita Rais wa Jamhuri ya Muunggano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba hawatafanikiwa.
“Kuna kundi dogo lenye tamaa na uchu wa madaraka linalosema eti ‘’SAMIA MUST GO’’ lipo ndotoni tena ndoto za Abunuwasi na halitafanikiwa kamwe kwa kuwa Rais Samia yupo na atakuwepo madarakani kwa mujibu wa Katiba inavyoeleza”, Mbunge Ndaisaba
0 Comments