Header Ads Widget

MBUNGE BUTONDO ATANGAZA HABARI NJEMA KWA WANANCHI WA KISHAPU


MBUNGE BUTONDO ATANGAZA HABARI NJEMA KWA WANANCHI WA KISHAPU

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo ametangaza habari njema kwa wakati wa jimbo hilo,kwamba tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kiwango cha lami kilomita 20, kutoka Kolandoto Manispaa ya Shinyanga hadi Mwangongo wilayani humo.

Butondo amebainisha hayo leo Septemba 13,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa shinyanga.
Amesema anaipongeza Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, kwa kuanza na kilomita 20 kati ya 63 hatua ambayo ni nzuri.

“Hii ni habari njema kwa wananchi wa kishapu,serikali imeshatoa fedha kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilomita 20 kutoka Kolandoto hadi Mwangongo,”amesema Butondo.
“Msisitizo wangu ni kwamba Ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na wakala wa barabara Tanroads wazifuatilie fedha hizo ili ujenzi uanze mara moja,”ameongeza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho, amempongeza Rais Dk,Samia Suluhu Hassan, kwamba ndani ya miezi mitatu katika Mkoa huo, ameshatoa fedha nyingi ukiwamo pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilomita 75, kutoka Kahama hadi Kakola yenye thamani ya sh.bilioni 101.2.
Amesema kwa upande huo huo wa ujenzi wa miundombinu ya barabara, Rais Samia ametoa tena sh.bilioni 14.3 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja, pamoja na kuyakarabati yale ambayo yaliathiriwa na mvua.

Aidha, kikao hicho kimejadili mambo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga na wananchi kwa ujumla, yakiwamo masuala ya kuimarisha kilimo cha zao la Pamba, kwa wakulima kufanya kilimo chenye tija.
kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments