Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha akizungumza kwenye semina ya Bodi ya maji bonde la kati
Suzy Butondo, Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha amewataka Wakulima na wafugaji kutunza vyanzo vya maji ili visikauke,na kusababisha malalamiko kutokana na kukosekana kwa maji katika maeneo mbalimbali, ambapo pia amewakumbusha bodi ya maji bonde la kati na wadau wote waendelee kuongeza vyanzo vya maji ili wananchi wapate maji ya kutosha.
Macha aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa maji kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na Bodi ya maji Bonde la kati, na kuwahusisha wadau mbalimbali wa maji iliyofanyika mjini Shinyanga, ambapo aliwataka wakulima na wafugaji wasiharibu vyanzo vya maji vilivyopo, badala yake wapewe elimu ili wafuate sheria za rasilimali za maji zinazotakiwa kufuatwa.
Amesema tatizo lililopo watu wengi wanaishi bila kuzijua sheria,hivyo ni vizuri wadau mbalimbali wa maji wanaopata mafunzo haya wajadili vizuri ili kuweza kuona ni jinsi gani wanalinda vyanzo vya maji ili visiendelee kuharibika.
"Niwaombe wawakilishi wote wa wakulima na wafugaji mkawaeleze wenzenu kuhusu sheria za maji mlizojifunza hapa leo kwani tatizo lililopo watu wengi hawajui sheria za maji, hapa tumeambiwa kwenye takwimu kwamba vyanzo vya maji vimepungua kutokana na watu kuharibu haribu vyanzo vya maji na kusababisha vyanzo hivyo kukauka kabisa"amesema Macha.
"Niwaombe Bodi ya bonde la kati na wadau wote mhakikishe wananchi wanapata maji kwa ubora zaidi,kwani sera ya maji inasema mama apate maji kwa umbali usiozidi mita 400 kwa sasa tuna asilimia 72 kwa Shinyanga mjini na vijijini asilimia 69 tunatarajia ifikapo mwaka 2025 mjini tutakuwa na asilimia 95 na vijijini 85 ya kupata maji"ameongeza Macha.
"Niwaombe muweke umuhimu wa kuratibu matumizi ya maji kwa sababu maji ni mtambuka, hivyo ni vizuri kuangalia ni wapi tunaongeza vyanzo vya maji na niombe uwekezaji uongezeke katika sekta ya maji,"amesema Macha.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kufanya jitihada za upatikanaji wa maji kwa ajili ya kumtua ndoo mama, na sasa imetoa shilingi Bilioni 77 ili kuhakikisha maji yanapatikana ambapo katika halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga zimetolewa jumla ya shilingi bilioni 48 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji, ikiwa ni pamoja na manispaa kuna mradi upo hatua za ununuzi, na ukikamilika manispaa itakuwa na asilimia 100 ya maji.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii mkuu Bonde la kati Halima Faraji amesema akifundisha sera na sheria ya usimamizi wa Rasilimali za maji amesema maji ni rasilimali muhimu kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi, ambapo sekta ya maji imegawanyika katika sekta ndogo mbili ambazo ni rasilimali za maji na huduma za usambazaji wa maji na usafi wa mazingira.
Amesema sera ya maji inaongozwa na sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 (NAWAPO) sheria za maji kanuni na miongozo mbalimbali , lengo la NAWAPO kuhakikisha usimamizi madhubuti wa rasilimali za maji na utoaji wa huduma endelevu za maji na usafi wa mazi gira vijijini na mijini.
Amesema sheria namba 11/2009 sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji ina sehemub16 vifungu 114, na sheria hii ni pamoja na mambo mengine imeainisha masuala ya kitaasisi kuzuia na kudhubiti uchafuzi wa maji, kuunda bodi za maji (Taifa, Bonde na eneo vidakio vya maji) makosa na adhabu
Fundi sanifu maji Israel Chafumbwe kutoka bonde la kati akiwasilisha majukumu mbalimbali ya bodi za maji alisema yanatakiwa kuandaa mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji,miradi, bajeti na mkakati wa utekelezaji wa bonde, kuunganisha mipango ya wilaya kwenye mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji ya bonde, kutoa miongozo na viwango vya ujenzi na matengenezo ya miundo ya vyanzo vya maji.
Afisa maji bonde la kati Shinyanga ambaye pia ni Kaimu mkurugenzi bodi ya maji Bonde la kati Kagoma Julius Mbaraka amesema pamoja na wajumbe kuwa pamoja na mambo mengine wamekutana katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Kidaka Maji cha Sibiti (Sibiti Catchment Committee) ili kufanya uchaguzi wa viongozi pamoja na kuandaa mpango kazi utakaotumika kuongoza utendaji kazi wa Bodi itakayoundwa.
Aidha baada ya mafunzo hayo ulifanyika uchaguzi wa kupedekeza jumuiya za watumia maji, mamlaka za maji, Halmashauri za wilaya, watumia maji, na sekta binafsi ambao walipendekezwa.
Afisa maendeleo ya Jamii mkuu Bonde la kati Halima Faraji akiwasilisha mada ya sera ya sheria ya maji
Afisa maendeleo ya Jamii mkuu Bonde la kati Halima Faraji akiwasilisha mada ya sera ya sheria ya maji
Afisa maendeleo ya Jamii mkuu Bonde la kati Halima Faraji akiwasilisha mada ya sera ya sheria ya maji
Fundi sanifu maji Israel Chafumbwe akiwasilisha mada ya majukumu mbalimbali za bodi za maji
Fundi sanifu maji Israel Chafumbwe akiwasilisha mada ya majukumu mbalimbali za bodi za maji
Afisa maji bonde la kati Shinyanga Kagoma Julius Mbaraka akiwa na mkurugenzi wa Kishapu Emmanuel Johnson
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
Tabora Singida na Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha
0 Comments