Michuano ya Dkt. Samia, Katambi Cup imeendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali ndani ya manispaa ya Shinyanga katika hatua ya 16 bora kuelekea kumtafuta mshindi atakayejinyakulia Shilingi Milioni 6.
Mashindano hayo yameendelea siku ya leo Agosti 07, 2024 ambapo timu ya Mwamalili FC imeichakaza timu ya Lubaga FC kwa mikwaju ya penati 4 kwa 3 mchezo uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Ufaransa kwa matokeo hayo timu ya Mwamalili FC imefanikiwa kusalia kwenye mashindano hayo.
Kwingineko ni timu ya Old Shinyanga imetolewa kwenye mashindano kwa kukubali kichapo cha goli 3 - 2 kutoka kwa timu ya Masekelo mchezo uliokuwa kupigwa katika uwanja wa Jasko uliopo kata ya Ngokolo.
Mashindano hayo yanatarajia kuendelea hapo kesho yakizikutanisha timu nne ambazo ni Kashwasa FC dhidi ya Bodaboda FC na Chamagua dhidi ya Ndala FC kuanzia muda wa saa 9 alasiri.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464