MWENGE WA UHURU UMEZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA KWA KISHINDO
MWENGE wa uhuru umezindua,kuona na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo manispaa ya Shinyanga, huku ukizindua shule mpya ya Sekondari Ndembezi.
Mwenge huo wa uhuru umeanza kukimbizwa leo Agosti 11,2024 katika Manispaa ya Shinyanga, ukitokea wilayani Kishapu na kukimbizwa umbali wa kilomita 74.5 na kumulika miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 4.2.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava akizungumza kwenye miradi hiyo, ameomba ilindwe pamoja na kuitunza miundombinu ya shule mpya ya
Sekondari Ndembezi.
"Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo ilindwe na kutunzwa ikiwamo na miundombinu mbinu ya shule hii ya Sekondari Ndembezi,"amesema Mnzava.
Aidha,amewasisitiza pia watalaamu wa halmashauri,kwamba waendele kuisimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu ili itekelezwe kwa ufanisi na kiwango kinachotakiwa.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjinj Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,ajira vijana na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye mbio hizo za mwenge wa uhuru, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi jimboni kwake na miradi mingi imetekelezwa.
Aidha,miradi ya maendeleo ambayo imepitiwa na mwenge huo wa uhuru, ni uzinduzi wa daraja la Kitangili, Ibinzamata na Iwelyangula, huduma za lishe,utunzaji wa mazingira,matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa soko kuu, uzinduzi wa klabu za rushwa shuleni, mradi wa vijana, uendelezaji mradi wa maji Bugayambelele, na uwekaji jiwe la msingi ukarabati wa hospitali ya manispaa ya Shinyanga.
Mwenge huo wa uhuru kesho utakimbizwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ukiwa na kauli mbiu isemayo"tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikaliza mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava akigawa vyandarua kwa wanawake wajawazito katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga alipowasili kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje.
0 Comments