Benki ya CRDB imekabidhi madawati 44 kwenye shule ya Sekondari Maganzo, iliyopo wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga ikiwa ni jitihada za Benki hiyo kuendelea kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo Agosti 30,2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawakilishi wa benki, wadau, wanajamii, walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba, ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya juhudi za benki hiyo kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini.
Amebainisha kuwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha kuwa asilimia 49.1 ya Watanzania ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, na wengi wao wanahitaji huduma bora za elimu ili kufikia malengo yao ya maisha.
“Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii kwa miaka mingi, tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya kijamii, hususan katika sekta ya elimu, mazingira, na afya kila mwaka, tunatenga asilimia moja ya faida yetu baada ya kodi kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii, na leo tunakabidhi madawati haya 44 ili kuwasaidia wanafunzi wa Sekondari ya Maganzo kupata mazingira bora ya kusomea,” amesema Chabba.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, alieleza kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuboresha elimu.
“Mwezi Aprili mwaka huu, tulikabidhi madarasa mawili pamoja na madawati katika Shule ya Msingi Kiloleli hapa Kishapu tunaendelea kurudisha asilimia moja ya faida yetu kwa jamii kwa kusaidia kilimo, elimu, afya, na mazingira,” amesema Wagana.
Ametoa wito kwa wanafunzi kutunza madawati hayo ili yaweze kudumu na kusaidia vizazi vijavyo, huku akisisitiza umuhimu wa wanafunzi na wananchi kufungua akaunti za CRDB kwa ajili ya kupata huduma bora za kifedha.
“Tunatoa mikopo yenye riba ndogo sana kwa wateja wetu, na tunawaomba muendelee kutuunga mkono kwa kufungua akaunti na kutumia huduma zetu,” amesema Wagana.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, ambaye ni mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Fatma Mohamed, ameipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu.
Amesisitiza kuwa mchango wa benki hiyo umekuwa wa manufaa makubwa kwa Wilaya ya Kishapu, na amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao.
“Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, napenda kutoa pongezi za dhati kwa Benki ya CRDB kwa juhudi zenu za kusaidia sekta ya elimu na nyinginezo hapa wilayani mnatoa mfano mzuri wa kujitolea kwa jamii, na tunaomba wadau wengine waige mfano huu ili kusaidia juhudi za serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania,” amesema Bi. Fatma.
Aidha, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maganzo, Mwalimu Evalisti Luhende, ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo, akibainisha kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,237, lakini imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa madawati 403.
Mwalimu Luhende ameeleza kuwa msaada huo utaenda mbali katika kupunguza changamoto hizo na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Wazazi na walezi waliokuwepo kwenye hafla hiyo wameipongeza Benki ya CRDB kwa kujali maendeleo ya watoto wao, huku wanafunzi wa shule hiyo wakiahidi kuongeza bidii katika masomo yao ili kufikia malengo yao na kuleta matokeo mazuri.
Madawati hayo ni sehemu ya mradi wa Keti Jifunze unaotekelezwa na Benki ya CRDB kwa lengo la kupunguza uhaba wa madawati nchini, na shule ya Maganzo sasa imekuwa moja ya wanufaika wa mradi huo.
Benki ya CRDB imeahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na shule nyingine mkoani Shinyanga katika juhudi za kuboresha sekta ya elimu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Fatma Mohamed, akiipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Fatma Mohamed, akiipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu.
Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi viti na meza 44 katika shule ya sekondari Maganzo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 30,2024.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi viti na meza 44 katika shule ya sekondari Maganzo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 30,2024 ambapo amewasisitiza wazazi, wanafunzi, walimu na watumishi wa umma kwa ujumla kufungua akaunti za CRDB ili kupata huduma bora za kifedha.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi viti na meza 44 katika shule ya sekondari Maganzo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 30,2024.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi viti na meza 44 katika shule ya sekondari Maganzo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 30,2024 ambapo amewasisitiza wazazi, wanafunzi, walimu na watumishi wa umma kwa ujumla kufungua akaunti za CRDB ili kupata huduma bora za kifedha.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maganzo, Mwalimu Evalisti Luhende akisoma taarifa ya shule hiyo Agosti 30,2024.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maganzo, Mwalimu Evalisti Luhende akisoma taarifa ya shule hiyo Agosti 30,2024.
Viongozi mbalimbali ambapo hafla ya kukabidhi viti na meza katika shule ya sekondari Maganzo ikiendelea.
0 Comments