NENDENI MKAHAMASISHE MATUMIZI SAHIHI YA UPIGAJI SIMU NAMBA 115 - DR. NDUNGILE.
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Msaidizi - Afya Mkoa wa Shinyanga Dr. Yudas Lucas Ndungile amewataka Waelishaji Jamii ngazi ya Halmashauri na Mkoa wa Shinyanga pamoja na majukumu mengine kwenda kutoa elimu ya matumizi sahihi ya upigaji wa namba ya dharura kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa akinamama wajawazito na watoto wadogo huku akisisitiza matumizi ya takwimu kwa ajili maamuzi na taarifa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Dr. Ndungile amebainisha hayo jana julai 12,2024 wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waelimishaji jamii hao katika ukumbi wa Vigmark Hotel ambapo pamoja na mambo menginw, lakini pia amewataka watalaam hawa kwenda kusimamia kikamilifu, kwa utu na uzalendo zaidi utolewaji wa huduma za dharura kwa walengwa na kwamba watumie elimu na maarifa wanayoyapata leo hapa kwenda kuongeza ufanisi zaidi ili lengo la uwepo wa huduma hii ukaonekane kama ambavyo Serikali inatarajia.
"Nendeni mkahamasishe matumizi sahihi ya upiga wa namba 115 kwa ajili ya kupata msaada wa dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wadogo ili wananchi waelewe vema kuwa, namba hii inapigwa tu pale ambapo jambo hilo linetokea kwa dharura na siyo vinginevyo," amesema Dr. Ndungile.
Kando na hayo, pia Dr. Ndungile amesema kuwa ni muhimu sasa kwenda kuongeza idadi ya madereva katika ngqzi ya jamii ili kuboresha utoaji huduma na pia kuongeza ajira kwao kwani uwepo wa nafasi na huduma hiyo ni fursa katika maeneo yao.
Akiwafafanulia umuhimu na lengo la uwepo wa program hii ndg. Stanley Kajuna ambaye ni Mwezeshaji wa Kitaifa amesema kuwa M-mama inamsaidia mama mjamzito au mtoto aliyepata changamoto ya dharura na kupiga namba ya simu 115 ili usafiri uweze kumfuata kwa haraka na kumpeleka katika kituo cha afya kilichopo karibu yake na aweze kuhudumiwa huku akisisitiza kuwa walengwa wasisubirie mpaka mgonjwa azidiwe ndiyo wapige simu, hapana.
Mafunzo haya ya siku moja yamekusudia kuwajengea uwezo waelimishaji Mkoa wa Shinyanga yaliyosimamiwa kwa ushirikiano wa ndg. William Mambo kutoka TAMISEMI - AFYA na Dr. Charles Kato ambaye ni Mratibu wa program hii Kanda ya Ziwa yamelenga kuongeza uelewa kuhusu mfumo wa m-mama, kuwawezesha washiriki kuwa na ujuzi na uwezo wa kuhamasisha jamii katika mfumo wa m-mama kwa ufanisi na kutengeneza mpango kazi wa utekelezaji
0 Comments