- Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi Mashuka na vyandarua katika Zahanati ya Didia halmashauri ya Shinyanga vijijini
- Suzy Butondo, Shinyanga press blog
- Mbunge viti maalumu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava amekabidhi mashuka na vyandarua katika zahanati ya kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga na katika Zahanati ya Didia halmashauri ya Shinyanga , ambapo pia amekabidhi mipira na jezi katika shule ya Kaselya sekondari kata ya Mwamala.
Akikabidhi vifaa hivyo leo Julai 5,2024 Mnzava amesema ametoa mashuka na vyandarua hivyo kufuatia kampeni ya kuzuia malaria kwa watoto, wanawake wajawazito, wazee wenye umri wa miaka 60 na wenye virusi vya ukimwi ambao mfumo wa kinga zao ni mdogo, ili kuhakikisha wanajikinga na malaria.
Mnzava amesema wanasaidia vitendea kazi hivyo kupitia mpango wa kudhibiti Malaria, hivyo anaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuzuia Malaria na kuhakikisha makundi hayo yanakuwa salama.
"Tunasaidia makundi haya ili yasipate ugonjwa wa Malaria, na kulingana mimi nipo kwenye kamati ya afya ya bunge nitaendelea kusaidia ili kuhakikisha makundi haya yako salama, hata mama Samia Suluhu anajitoa nakusafiri kwa ajili yakutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama, kwa kutafuta fedha za kujenga zahanati vituo vya afya na hospitali"amesema Mnzava.
Aidha wakati akikabidhi Mipira na Jezi kwa wanafunzi wa shule ya Kaselya amewataka waendelee kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi ni afya yanazuia magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza, yanasaidia mfumo wa mishipa ya fahamu na yanasaidia kurudisha kumbukumbu.
"Pia naomba niwatie moyo wanangu wa kiume na wakike kwamba mkaze buti katika masomo na mtunze malengo yenu, msikubali kushawishiwa na watu waharibifu, kwani sasa hivi kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili, watoto wengi wa kike wanadanganywa nawatoto wa kiume wanarawitiwa wakija watu wa kuwadanganya msikubali ili muweze kutimiza ndoto zenu za baadae"amesema Mnzava.
"Humu humu tunahitaji kupata madaktari wahasibu,wanajeshi,wanasheria, madiwani, wabunge, mawaziri na Rais, hivyo someni kwa bidii ili kuhakikisha mnatimiza malengo yenu ya kuja kuitwa baba na wa kike mjitunze muda ukifika mtafanya mambo yenu jifunzeni kusubiri msije kupata mimba za utotoni au magonjwa "ameongeza Mnzava.
Mnzava pia aliwataka wanananchi wote wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili waweze kupata haki yao ya kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, pia amewaomba wanawake wenye uwezo wa kugombea wajitokeze kugombea nafasi za serikali za mitaa wasiogope kwa sababu hi haki yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu aliwataka wanawake wapendane, wasioneane wivu wahamasishane wagombee uongozi wa serikali za mitaa, pia amewataka wazazi kulinda maadili ya watoto,na wanawake watimize majukumu yao kwa wenza wao.
"Namshukuru sana Mheshimiwa mbunge wetu kwa kutukumbuka na kutuletea vifaa hivi katika hospitali yetu ya Kizumbi na hospitali ya Didia Mungu ambariki vifaa hivi vitawasaidia watu wote bila kujali huyu ni chama gani wakija hapa hospitali watajifunika mashuka wote, hivyo tuendelee kumuombea mbunge wetu ili aendelee kufanya makubwa zaidi"amesema Bizulu.
Baadhi ya wanawake waliopatiwa neti akiwemo Lusia Dotto Mkazi wa Kizumbi walimshukuru Mnzava kwa kuwasaidia vyandarua na mashuka ambapo waliahidi kwamba wataendelea kuzaa watoto kwa sababu viongozi wao wanawasaidia.- Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akisaini kitabu katika ofisi ya CCM kata ya Mwamala
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akivalishwa skafu baada ya kupokelewa katika kata ya Didia
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza katika kata ya Didia

Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi jezi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kaselya
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi jezi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kaselya
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi Mashuka na vyandarua katika Zahanati ya Didia halmashauri ya Shinyanga vijijini
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza katika kata ya Didia
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi Mashuka na vyandarua katika Zahanati ya Didia halmashauri ya Shinyanga vijijini
Mbunge viti maalumu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akikabidhi Mashuka na vyandarua katika Zahanati ya Didia halmashauri ya Shinyanga vijijini
Mbunge viti maalumu akimkabidhi mtoto Chandarua
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza
Mwalimu wa michezo katika shule ya sekondari Mwamala akimshukuru mbunge viti maalumu Christina Mnzava kwa kupeleka vifaa vya michezo
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT mkoa wa Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Sharifa Mdee akizungumza
Katibu wa UWT Shinyanga vijijini Magdalena Dodoma akizungumza
Dkt. wa zahanati ya Kizumbi Bernadetha Mapunda akishukuru kwa vitendea kazi alivyokabidhiwa
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akizungumza
Mwenyekiti wa Wanawake Samia mkoa wa Shinyanga Husina Ally akizungumza
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji UWT mkoa wa Shinyanga
Mbunge viti maalumu akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Kaselya kata ya Mwamala
Mbunge viti maalumu akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kaselya kata ya Mwamala

Kazi ikiendelea
Mbunge viti maalumu Christina Mnzava akiwa amebeba mtoto baada ya kukabidhi vyandarua katika Kata ya Kizumbi
Viongozi wa kikundi cha wanawake Samia mkoa wa Shinyanga
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464