Header Ads Widget

WANACHUO 64 WAHITIMU MAFUNZO ELIMU YA UFUNDI STADI VETA SHINYANGA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Ngazi ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 64 kati yao wavulana 45 na wasichana 19 wamehitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi na Ufundi wa Mitambo mikubwa.

Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Juni 7,2023 ambapo mgeni rasmi Afisa Tarafa, Tarafa ya Samuye , Aron Laizer akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mgeni rasmi Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer amepongeza jitihada za Serikali chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini kwani vyuo vya ufundi stadi vimekuwa msaada mkubwa katika maendeleo ya taifa na wananchi wake hasa wakati huu ambapo serikali inahimiza suala la uwekezaji katika viwanda.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer.

“Taifa letu sasa lipo katika harakati za kuhamasisha ujenzi wa viwanda ambapo nguvu kazi yake kubwa inategemea wahitimu kutoka vyuo vya VETA. Tatizo la ajira kwa vijana wengi wanaohitimu elimu ya msingi, sekondari na vyuo suluhisho lake ni juu ya mafunzo ya elimu ya ufundi stadi/mafunzo ya amali ambapo ndipo stadi mbalimbali hutolewa ili mtu aweze kujiajiri na kuajiriwa ili kuongeza kipato na kukuza pato la taifa”,ameeleza Laizer.

Ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi pamoja na vijana kutumia chuo hicho kujiunga na kozi mbalimbali ili kuleta maendeleo katika mkoa na taifa kwa ujumla huku akiwahamasisha wahitimu kuunda vikundi ili wapate mikopo inayotolewa kwenye halmashauri za wilaya.

Aidha mara baada ya kutembelea karakana ya ukataji madini vito katika Chuo cha VETA Shinyanga, Laizer amefurahia na kukipongeza chuo hicho kuanzisha kozi ya Madini na kukiomba chuo hicho cha VETA kuendelea kubuni kozi mbalimbali kulingana na mahitaji ya jamii.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer  (wa nne kulia) akiwa katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

“Kuhusu ombi la kupatiwa kituo cha polisi katika eneo hili nimelichukua kwa ajili ya kushirikisha vyombo vinavyohusika. Pia tayari ofisi ya Mkuu wa wilaya kupitia Uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inashughulikia changamoto ya usafiri wa umma kwa wanachuo na wafanyakazi ili kuanzisha route ya daladala itakayohudumia maeneo ya Kizumbi. Hali kadhalika serikali inaangalia moja ya zahanati zilizopo maeneo haya kama zinaweza kupandishwa hadhi ili kutoa huduma bora. Changamoto zingine zitaendelea kushughulikiwa na VETA makao makuu”,ameongeza Laizer.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele amesema chuo hicho ni miongoni mwa vyuo 72 vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania ambapo sasa kinatoa mafunzo ya ufundi Stadi katika fani 10 za muda mrefu na kozi zaidi ya 27 za muda mfupi kikiwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 400 kwa kozi za muda mrefu na wanafunzi zaidi ya 600 wa kozi za muda mfupi kwa wakati mmoja.

Mabelele amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya kuharibika kwa uzio wa chuo hivyo kuhatarisha usalama wa wananchuo na mali huku akiiomba serikali kujenga kituo cha polisi ili kusaidia usalama wa watu na mali zao katika eneo la chuo cha VETA Shinyanga, kujengwa kwa kituo cha afya jirani na chuo pamoja na usafiri wa umma kwa ajili ya wafanyakazi na wanachuo.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele.

“Wahitimu mnaomaliza mafunzo yenu naomba mkatuwakilishe vyema kwenye taasisi mbalimbali. Mnapoelekea huko sitaki kusikia mnaenda kukaa nyumbani bali nendeni mkafanye kazi. Sisi tunapokupa ujuzi tunataka ukautumie kufanya kazi badala ya kukaa tu. Mnapotoka hapa msiende kukaa na ujuzi, nendeni mkajiajiri, kazi zipo mtaani na wapo watu wa kuunga mkono kazi mnazofanya. Mkaende kuishi kwenye maisha ambayo yatawafanya mpate ajira”,ameongeza Mabelele.

Katika hatua nyingine amewaomba wazazi na walezi waendelee kupeleka watoto waende wakajifunze mafunzo ya ufundi stadi kwani chuo hicho kina kozi mbalimbali nzuri ikiwemo kozi ya ukataji madini vito na fani ya ufundi wa mitambo mikubwa.

Mkuu huyo wa Chuo cha VETA Shinyanga ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa anaoufanya kwenye sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi/amali kwani juhudi hizo zimekuwa chachu ya kutoa mafunzo hivyo kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi kwa gharama ndogo bila kubagua jinsi, hali ya uumbaji na mahitaji maalumu.
Sehemu ya Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III)

Naye Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye amesema mpaka sasa chuo hicho kina wanafunzi 468 wa kozi za muda mrefu kati yao 295 ni wavulana na 173 ni wasichana waliodahiliwa kuanzia Januari mpaka Juni 2024, kwa kozi za muda mfupi idadi yao ni 665 kati yao 619 ni wavulana na 46 ni wasichana.

Amezitaja Fani 10 Ndefu zinazotolewa katika Chuo cha VETA Shinyanga kuwa ni Fani ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics), Fani ya Umeme wa Nyumbani (Electrical Installation) , Fani ya Useremala (Carpentry and Joinery), Fani ya Uchomeleaji na uundaji vyuma (Welding and Metal Fabrication), Fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo (Designing, Sewing and Clothing Technology), Fani ya Bomba (Plumbing and Pipe Fitting), Fani ya Ujenzi (Masonry and Bricklaying), Fani ya Uhazili na Tehama (Secretarial and Computer Application), Fani ya Uendeshaji Mitambo (Plant Operation) na Fani ya Ukataji, Ung’arishaji na Uchoangaji wa Madini ya Vito (Gemstone cutting,polishing and carving).
Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye.

Pia Chuo cha VETA Shinyanga kinatoa Mafunzo ya Muda mfupi katika fani 27 ambazo ni Fani ya magari, Fani ya umeme wa majumbani, Useremala, uungaji vyuma, ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo,mabomba,ufundi uashi, uhazili na Tehama,uendeshaji mitambo,udereva, urembeshaji na mapambo, Tehama, umeme wa magari na utengenezaji wa batiki.

Fani zingine ni Madini (uchimbaji na ulipuaji miamba), upishi, usukaji wa motor, ufundi pikipiki, utengenezaji wa mitambo mikubwa,ufundi jokofu na viyoyozi, utengenezaji wa mitambo mikubwa,kudarizi, udereva wa bajaji na pikipiki,ufundi Kompyuta na ufundi mitambo mikubwa.

Ntahigiye amesema VETA Shinyanga imefanikiwa kushirikiana na Taasisi, Makampuni, Mashirika ya Serikali na yasiyo ya kiserikali kwa kuwapatia wanachuo sehemu za kufanya mafunzo kwa vitendo (Field Attachment) na kufanikiwa kulinda na kutunza mazingira ya chuo.

Akisoma risala ya wahitimu, Asia Ally amesema wamekuwepo katika chuo hicho kwa mwaka mmoja na wamefanikiwa kupata mafunzo ya ufundi stadi, wanaondoka chuoni wakiwa na ujuzi wa kutosha, watakwenda kujiajiri na kuajiri wengine wakijiamini kwa kufanya kazi kwa weledi bila kusimamiwa na mtu yeyote kwa ukaribu. 

ANGALIA PICHA MATUKIO WAKATI WA MAHAFALI
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer  (katikati) akisikiliza maelezo katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 7,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele (wa nane kulia) akielezea namna wanavyokata madini katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga 
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele (kulia) akielezea namna wanavyokata madini katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga 
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer  (wa nne kushoto( akiwa katika Karakana ya Umeme katika Chuo cha VETA Shinyanga wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer  (kushoto) akiwa katika Karakana ya Umeme katika Chuo cha VETA Shinyanga wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer  akizungumza wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele akizungumza wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho
Mhitimu Asia Ally akisoma risala ya wahitimu
Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi na Ufundi wa Mitambo mikubwa wakiwa kwenye mahafali

Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) wakicheza muziki

Awali Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) wakiingia ukumbini
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele (kulia) akifurahia jambo na Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye wakati wa mahafali
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wanafunzi wa fani ya Urembeshaji na Mapambo wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wanafunzi wa fani ya Urembeshaji na Mapambo wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mwalimu wa kujitolea  Canada katika Chuo cha VETA akitoa neno kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mwalimu wa kujitolea  Comoro katika Chuo cha VETA akitoa neno kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mmoja wa wazazi akitoa neno kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 

Wageni waalikwa, Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Aron Laizer akikabidhi cheti kwa mmoja wa Wahitimu wa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika chuo cha VETA Shinyanga

Wazazi , wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu

Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Zoezi la zawadi likiendelea kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wahitimu wakimpatia zawadi ya kuku Mkuu wa Chuo cha VETA Magu Mabelele kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wanafunzi wa VETA, wageni waalikwa, wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 
Wanafunzi wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 42 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu 

Mgeni rasmi, wageni waalikwa wakipiga picha ya kumbukumbu

Mgeni rasmi, wahitimu wakipiga picha ya kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments