Header Ads Widget

CHADEMA SHINYANGA WALALAMIKA KUNYIMWA UWANJA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA

CHADEMA SHINYANGA WALALAMIKA KUNYIMWA UWANJA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mwenyekitiwa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila.

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Shinyanga Mjini, kimelilalamikia Jeshi la ZimaMoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga,kuwanyima Uwanja kwa ajili ya kufanya Mkutano wao wa hadhara,Uwanja ambao mara nyingi hutumika kwa ajili ya Mikutano mbalimbali.

Malalamiko hayo yametolewa leo Juni 8,2024 na Viongozi wa Chadema wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari, juu ya kunyimwa Uwanja wa kwa ajili ya kufanya Mkutano wa hadhara na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Shinyanga.
Mwenyekitiwa Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, amesema Juni Mosi mwaka huu waliandika barua kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kwa ajili ya kuomba Uwanja ili Juni 7 wafanye Mkutano wa hadhara, lakini katika barua yao wakajibiwa siku hiyo Uwanja huo utakuwa na Shughuli nyingine.

Amesema baada ya kupewa majibu hayo wakaandika barua nyingine ya kuomba Uwanja huo, ili wafanye Mkutano wa hadhara Siku ya Jumatano ambayo ni juni 12 mwaka huu, lakini wakapewa majibu kwamba Uwanja huo sasa hivi hautumiki tena kwa shughuli za kisiasa, bali utatumika kwa shughuli za Majeshi naza kiserikali,hivyo watafute Uwanja mwingine.
“Majibu ambayo tumepewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia barua zao hizi mbili kuna uwalakini, mara Uwanja utakuwa na Shughuli nyingine, tukasogeza siku mbele wakajibu tena Uwanja huo hautumike tena Kisiasa, hapa inaonyesha kwamba katika Mkoa wa Shinyanga kuna ukandamizwaji wa Demokrasia,”amesema Ngunila.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi, amesema wanasikitika kunyimwa Uwanja huo,lakini Vyama vingine vya Siasa vimekuwa vikifanya Mikutano ya hadhara kwenye Uwanja huo huo, ila wao ndiyo wanawekewa mapingamizi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya.

“Ukiangalia Barua hizi Mbili za Zimamoto zina Majibu Tofauti, hapa inaonyesha kuna kitu au wamepokea maelekezo kutoka Juu, hata Tundu Lissu tumeshuhudia amekuwa wakinyimwa Viwanja vya kufanya Mikutano ya hadhara kwenye baadhi ya Mikoa, ina wezekana kuna Mikakati inatengezwa chini kwa chini,”amesema Ntobi na kuongeza,

“Mbona Mwaka jana tulifanya Mkutano wa hadhara kwenye Viwanja hivyo, kwa nini sasa hivi tuzuiwe hasa kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikaliza Mitaa, hivyo basi pamoja na mazuio yao sisi siku hiyo ya Jumatano ambayo ni Juni 12 tutafanya Mkutano hapo watake wasitake sababu zao hazina Mantiki wala Kisheria,”
Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala, alikiri ni kweli wamewazuia Chadema kufanya Mikutano ya hadhara kwenye Uwanja huo, na kufafanua kwamba zamani Uwanja huo hau kuwa chini ya Jeshi hilo, ndiyo maana ulikuwa ukitumika kwa shughuli zozote lakini sasa hivi upo chini yao.

Amefafanua kuwa baada Uwanja huo kuwa Chini ya Jeshi la Zimamoto Rasmi,kuna utaratibu ambao umewekwa kuwa Uwanja huo sasa hivi utatumika kwa Shughuli za Kijeshi naza Serikali, na siyo shughuli za kisiasa tena, huku akiwashauri Chadema ni vyema wakatafuta Uwanja mwingine.

Aidha,akijibu madai ya Chadema kwamba licha ya kuwanyima Uwanja huo, siku hiyo ya Jumatano lazima watafanya Mkutano wao wa hadhara bila ya kujali mazuio yao, amesema kwamba suala hilo lipo Nje ya Mamlaka yake bali watashughulika na Mamlaka zingine.

Post a Comment

0 Comments