Header Ads Widget

SHUWASA KUTEKELEZA MRADI MKUBWA WA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA WA EURO 120


SHUWASA KUTEKELEZA MRADI MKUBWA WA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA WA EURO 120

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAMLAKA ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA),wapo kwenye utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa utoaji huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira wenye thamani wa EURO 120.

Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, ambao unatekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza utatumia EURO 76.
Hayo yamebainishwa leo Juni 5,2024 kwenye Warsha ya Madiwani na Wadau wa Maji, katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambapo washiriki walielezwa namna Mradi huo utakavyotekelezwa.

Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusupu Katopola,amesema Mradi huo utamaliza kabisa tatizo la Maji katika Manispaa ya Shinyanga,ikiwamo na Miji ya Tinde,Didia na Iselamagazi ya wilayani Shinyanga ambayo hua wanaihudumia pamoja na kujenga Mitambo ya kuchakata Tope Kinyesi.
"Mamlaka yetu inatoa huduma kwa Wakazi 282,698,na Wakazi wapatao 189,580 ndiyo wanapata huduma ya Majisafi na salama, sawa na asilimia 67.1,"amesema Mhandisi Katopola na kuongeza

"Wastani wa Mahitaji ya Maji kwa Siku kwa wananchi ni Mita za Ujazo 19,288, lakini Maji ambayo tunasambaza kwa Siku ni Mita za Ujazo 14,936,na hii inatokana na Miundombinu tuliyonayo, hivyo kupitia Mradi huu wananchi wote watapata Majisafi na Salama."
Naye Mratibu wa Miradi kutoka SHUWASA Mhandisi Willfred Julius akiwasilisha taarifa ya utekelezwaji wa Mradi huo, amesema Serikali ya Tanzania imesaini Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD),kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa huduma ya Majisafi na usafi wa Mazingira.

Amesema Mradi huo umekadiriwa kugharimu kiasi cha EURO Milioni 120 na utatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo Awamu ya kwanza utatumia EURO Milioni 76, na Shirika la Maendeleo la Ufaransa litatoa EURO Milioni 75, na EURO Milioni 1 ni mchango wa Serikali ya Tanzania.
Amesema Mradi huo pia utaboresha Miundombinu ya Usafi wa Mazingira,ujenzi wa Mitambo ya kuchakata Tope Kinyesi katika maeneo ya Ihapa,Kituli,Mwagala,na Mwamakalanga.

Amesema watajenga pia vyoo 36 katika Maeneo ya Shule,Soko, na Vituo vya Afya, na kwamba katika Manispaa ya Shinyanga watajenga vyoo 31,Didia Viwili,Tinde kimoja na Iselamagazi Viwili.
Pia, amesema kupitia Mradi huo watafanya ukarabati wa Chanzo cha Maji Bwawa la Ning'hwa,kwa kufanya upanuzi ili liwe na uwezo Mkubwa wa kutoa huduma ya maji, na kwamba bwawa hilo lilijengwa Mwaka 1972 na lilifanyiwa ukarabati wa mwisho mwaka 1984.

Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga ambaye amemwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro,ameipongeza SHUWASA kwa kushirikisha Madiwani na wadau wa Maji juu ya Mradi huo, na kwamba uongozi bora ni pamoja na kuwepo na uwazi wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Ameendelea kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kutoa huduma ya Maji kwa wananchi,na kwamba miaka ya nyuma Mji wa Shinyanga ulikuwa na shida kubwa ya maji, lakini sasa hivi shida hiyo haipo tena, huku akimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kutafuta fedha na kutekelezwa Miradi mikubwa ya Maji.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza kwenye Warsha hiyo na kuelezea utekelezaji wa Mradi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Mratibu wa Miradi kutoka SHUWASA Mhandisi Willfred Julius akiwasilisha taarifa ya utekelezwaji wa Mradi huo.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Washiriki wakiendelea na Warsha.
Warsha ikiendelea.
Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akiwa na Madiwani katika moja ya eneo ambalo utajengwa Mtambo wa kuchakata Tope Kinyesi lililopo Mwagala Manispaa ya Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments