Header Ads Widget

RC MACHA APONGEZA UJENZI JENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA,NYUMBA ZA WATUMISHI

RC MACHA APONGEZA UJENZI JENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA,NYUMBA ZA WATUMISHI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameridhishwa na Ujenzi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pamoja na Nyumba za Watumishi.

Amebainisha hayo leo Mei 17,2024 alipotembelea kuona Maendeleo ya ujenzi huo katika Makao Makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga yaliyopo Kata ya Iselamagazi.
Amesema jengo hilo la Utawala limejengwa vizuri na ameridhika pamoja na nyumba za watumishi ambao watakaa Wakuu wa Idara.

"Nimeridhika na ujenzi wa Jengo hili la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pamoja na Nyumba za Watumishi mmefanya kazi nzuri,"amesema Macha.
Aidha,amesisitiza pia waendelee kujenga na nyumba zingine ambazo wataishi Watumishi wengine ili waishi karibu na kurahisha utendaji wa kazi.

Katika hatua nyingine,ameagiza ujenzi huo utakapokamilika,kwamba Samani za ndani (Furniture)wanunulie ndani ya nchi hasa katika Mkoa wa Shinyanga na siyo nje ya Nchi.
Ametoa Maagizo pia kwa Wakurugenzi wote Mkoani humo,kwamba katika ujenzi wa Majengo ya Serikali wajitahidi kununua vifaa vya Watanzania.

Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo akisoma taarifa ya ujenzi huo, amesema ulianza mwaka 2021 na hadi kukamilika kwake utagharimu Sh.bilioni 3.6, lakini hadi sasa wametumia Sh.bilioni 2 na ujenzi unaendelea.
Jengo la Utawala.
Ukaguzi ujenzi Nyumba za Watumishi.
Muonekano Moja ya Nyumba ya Watumishi.

Post a Comment

0 Comments