Header Ads Widget

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGIZA MIKATABA NA BIMA ZA AFYA KWA WAANDISHI WA HABARI KUTEKELEZWA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEAGIZA MIKATABA NA BIMA ZA AFYA KWA WAANDISHI WA HABARI KUTEKELEZWA

Na mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Mjaliwa metoa agizo kuboreshwa ustawi wa sekta ya habari nchini kwa kuhakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa katika maslahi ya afya na malipo ya wanahabari ili kuimarisha mazingira salama ya utendaji kazi.
 Ametoa agizo hilo leo Mei 3,2024 katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Tanzania,yaliyofanyka jijini Dodoma na kuwataka wadau wa sekta ya habari kusimamia bima za afya kwa waandishi wa habari.

" Ni agize wizara husika kufanya kikao na wadau kujadiliana kuhusu suala la bima ya afya kwa waandishi na vema wanahabari washirikishi vikao hivyo kutoa maoni yao" amesema Majaliwa.
Pia MajiwaAlisema sekta ya habari ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa, na kudumisha amani nchini hivyo ni vyema kuhakikisha waajiri wanawapa mikataba ya kazi itakayochagiza weredi mkubwa katika utendaji kazi.

" Suala la mikataba ya kazi kwa wanahabari ni vema vikao vya majadiliano vifanyike baina ya taasisi za habari na vyama vya wafanyakazi kwa ngazi zote ili kuweka mazingira salama ya sekta" alisema Majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu alisisitiza kuanzia sasa taasisi za serikali kuzingatia bajeti za vyombo vya habari katika shughuli zao na kulipa kwa wakati, huku akiwataka watendaji wa serikali kuwa na gari maalum la waandishi katika shughuli za serikali ili kuhakisha usalama wao.

Waandishi wa habari Tanzania zaidi ya asimilima 70 hawana mikataba ya kazi na hivi punde ,Mfuko wa bima ya afya uliondoa kifurushi za bima kwa ajili ya waandishi wa habari.
Kwa upande wake,Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania, Nape Nnauye, anasema,uchumi wa vyombo vya habari nchini ni duni na vingi vinashidwa kujiendesha, na jitihada za maksudi zisipochukuliwa kuvinusuru vitakufa.

Hata hivyo Nape amesema pamoja na madhira hayo ya kiuchumi, hali ya uhuru wa vyombo vya habari ni nzuri nchini na kuifanya Tanzania kuwa ya 97 na kutoka nafasi ya 124 kwa mujibu wa taarifa za World Press Freedom za mwaka 2024.
" ... na Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki", anasema Nnauye.

Nape alibainisha madeni ya vyombo vya habari kwa serikali ni Shilingi Bilion 18 na kudai ni vema wizara na taasisi za serikali kuanza kulipa kwa kuwa fungu kwa vyombo vya habari katika Kila sekta uwa lipo katika kila msimu wa bajeti.

Naye,Rais wa Umoja Klabu za Habari Tanzania,Deogratius Nsokolo anasema,Waandishi waliondolewa katika Mfuko wa Bima ya Afya bila kushirikishwa na kuwapa wakati magumu pindi wapatapo changamoto za kiafaya kutokana wengi wao kutokuwa na mikataba ya kazi, zaidi ya kutegemea fedha za mtoa habari.

"Awali kulikuwa na kifurushi cha wanahabari kutoka Mfuko wa Bima ya Afya na kilitolewa bila sie kushirikishwa kikamilifu na mazingira ya waandishi na magumu huku wakiwa hawana mikataba ya kazi"anasema Nsokolo.

Post a Comment

0 Comments