Header Ads Widget

WANAUME WAUZA MPUNGA MASHAMBANI NA KUKIMBILIA KWENYE KUNDI LA WANAWAKE MAOKOTO

Meneja mradi kutoka shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisingili kata ya Ilola 

Suzy Butondo, Shinyanga Press blog

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kisingili kata ya Ilola halmashauri ya Shinyanga wako hatarini kukumbwa na janga la njaa baada ya kata hiyo kuvamiwa na kundi la wanawake linalojiita kundi la maokoto, ambalo linasababisha wanaume wanauza mazao yao mashambani na kukabidhi fedha kwa wanawake hao.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na baadhi ya wananchi waliokuwa wakizungumza na Shirika la Rafiki SDO kwa ufadhili wa shirika la WFT lililotembelea kwenye kijiwe cha Kahawa katika kijiji hicho kwa lengo la kuwashirikisha wanaume katika mchakato wa kupinga ukatili dhidi ya. wanawake na watoto

Wakichangia hoja kwenye kijiwe cha Kahawa wananchi hao akiwemo Paul Mayanji na Masele Senga wamesema hali ni mbaya sana katika Kata ya Iloa kwani kata imevamiwa na kundi la  wanawake  linalojiita maokoto na kusababisha wanaume kuuzia mpunga mashambani bilakuwapa taarifa wenza wao.

"Kuna kikundi cha akina mama wanasema wamekuja kwenye maokoto,hivyo wanaume wanauzia mpunga mashambani, na akishauza anapotea nyumbani wiki mbili bila kujua familia yake yuko wapi, anarudi nyumbani baada ya fedha za mpunga kumwishia anauza tena magunia ya ndani yaliyobaki,"amesema Manyanji

Sheka Masingija mkazi wa kijiji cha Kasingili amesema anaiomba serikali iingilie kati suala hilo, kwani kuna hatari ya kutokea njaa kwa sababu kata imevamiwa na kundi hilo, ambapo wanaume wengi wamekuwa wakiuza mazao bila kuwashirikisha wenza wao ama watoto ambao ndiyo wanashinda shambani wakilima.

Tatu Lubinza ambaye ni Mwezeshaji ngazi ya jamii katika kata ya Ilola amesema wanawake wengi kwa sasa hawana amani na ndoa zao, kwani wanaume wanapouza kimya kimya mazao wanapotelea kwenye kundi linslojiita la maokoto wengine wanasingizia wamepata ajali.

"Kwa kweli tuna kilio kikubwa hapa kijijini wanaume wetu hawashikiki tena wanauza mpunga na wanakimbilia kwa kundi la maokoto hivyo sisi wanawake tunabaki na watoto tukipata shida tulilima tukizani tunamaliza matatizo ya njaa lakini imekuwa ni tofauti, wanaume wengi wamerukwa na akili kabisa, tunaomba mtusaidie tu nyinyi wadau wetu ili tatizo hili liweze kukomeshwa"amesema Mbuke Bundala.

Kwa upande wake meneja mradi wa SDO Maria Maduhu amewashauri wananchi washirikiane na viongozi kutengeneza taratibu upande wa sungu sungu ili wale wanaume wanaouza mazao mashambani na kupeleka kwenye kundi la maokoto wachukuliwe hatua kwa kupitia kanuni ndogo kwa kila kijiji.

"Lakini kinachotakiwa katika huduma ya kwanza sisi ambao ni waelewa tutoe elimu kwa hawa watu ili wasiendelee kuuza mpunga ili kuweza kuepuka njaa kwa watoto wetu na kusababisha magonjwa kwa familia"amesema Maria.

Kwa kuwa hili jambo limekithiri ssna huku kijijini ni vizuri kurudisha Shikome ili wanaume wansofanya uharibifu wasifanye tena washauriwe wakiwa kwenye shikome, na ili kufanikisha ni vizuri wanajamii mkahamasisha kianzishwe tena ili kuokoa kizazi.

Afisa Tathimini na ufuatiliaji Sospeter kutoka shirika la SDO amewashauri wanaume kuwa mabalozi, wazee wa heshima, viongozi wa dini wasaidie jamii wawe na nafasiza kutoa ujumbe ili ukatili huo usiendelee,kwani wakiebdeleakufanya hivyo hata watoto wanaoona ki achofanywa na wazazi nao watafanya hivyo,hivyoni vizuri kukemea hali hiyo.
Meneja mradi kutoka shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisingili kata ya Ilola 
Meneja mradi kutoka shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisingili kata ya Ilola 
Mmoja wa wananchi akichangia hoja  kwenye kijiwe cha kahawa
wananchi wakiendeleana majadiliano juu ya kundi la wanawake lililovamia kata  ya Ilola

Tatu Lubinza ambaye ni Mwezeshaji ngazi ya jamii katika kata ya Ilola 
wananchi wakiendeleana majadiliano juu ya kundi la wanawake lililovamia kata  ya Ilola
Wananchi wakiendeleana majadiliano juu ya kundi la wanawake lililovamia kata  ya Ilola

Afisa Tathimini na ufuatiliaji Sospeter kutoka shirika la SDO akifafanua jambo
Mmoja wa wananchi akichangia hoja  kwenye kijiwe cha kahawa
Mmoja wa wananchi akichangia hoja  kwenye kijiwe cha kahawa
Meneja mradi kutoka shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisingili kata ya Ilola 
Mmoja wa wananchi akichangia hoja  kwenye kijiwe cha kahawa
Afisa mradi Rafiki SDO Suleyman Abdalah akifafanua jambo kwenye kijiwe cha Kahawa
Afisa Tathimini na ufuatiliajiMadaga Joseph akifafanua jambo 
Wananchi wakiendeleana majadiliano juu ya kundi la wanawake lililovamia kata  ya Ilola
Afisa Tathimini na ufuatiliajiMadaga Joseph akifafanua jambo 
Afisa Tathimini na ufuatiliajiMadaga Joseph akifafanua jambo

Post a Comment

0 Comments