Header Ads Widget

KATAMBI AKABIDHI AMBULANCE MPYA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI


Katambi akabidhi Ambulance kuboresha huduma za afya kwa wananchi

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amekabidhi Gari la Wagonjwa (Ambulance), ambayo itatumika kutoa huduma Kituo cha Afya Kambarage.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, amekabidhi Ambulance hiyo leo April 27,2024 katika Stendi ya Magari Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga, na kushuhudiwa na Wananchi,Viongozi wa Serikali pamoja na Chama.
Amesema hiyo ni Ambulance ya pili ambayo ameitoa katika Ahadi zake, ambapo ya kwanza aliitoa February 8 Mwaka huu,na leo pia amekabidhi Ambulance nyingine ili kuendelea kuboresha huduma za Afya.

"Mimi nikiahidi natekeleza, Ambulance ambayo naikabidhi leo itatumika kutoa huduma Kituo cha Afya Kambarage na ile ilikuwa ya Kambarage sababu ni ndogo itakwenda Ihapa,"amesema Katambi.
Amemshukuru pia Rais Samia,kwa kuendelea kutoa fedha nyingi na kuboresha huduma za Afya kwa wananchi,pamoja na kutoa ajira za Afya na upatikanaji wa vifaa tiba.

Katika hatua nyingine amemshukuru Rais Samia,Makamu wa Rais,na Waziri Mkuu kwa miongonzo yao na kumwezesha kufanya kazi za Serikali pamoja na kuhudumia Wananchi wa Jimbo lake.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga (DMO) Dk.Elisha Robert,ameshukuru kupata Ambulance hiyo na kwamba sasa vimefika Nne,ambazo zitasaidia kubeba Wagonjwa na kuwawahisha kupata huduma za matibabu.

Amesema ndani ya miaka Mitatu ya Rais Samia katika Manispaa ya Shinyanga zimeshajengwa Zahanati Mpya Sita, na zingine Mbili zinaendelea kukamilishwa ikiwamo ya Mwamagunguli, pamoja na kutoa Ajira 93 za Watumishi wa Afya.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani, amempongeza Mbunge Katambi kwa kuendelea kupambania Wananchi katika suala zima la Maendeleo, na sasa ameendelea kutekeleza Ahadi yake ya kuleta Magari ya Wagonjwa.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, ametoa wito kwamba Magari hayo ya Wagonjwa ambayo yamekabidhiwa na Mbunge kwamba wayatunze pamoja na Madereva kuyaendesha vizuri na kutosababisha Ajali.

Post a Comment

0 Comments