Header Ads Widget

TGNP YAWAPATIA UJASIRI WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI KIJIJI CHA KILOLELI WILAYANI KISHAPU WAONDOKANA NA UTEGEMEZI

TGNP YAWAPATIA UJASIRI WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUONDOKANA NA UTEGEMEZI KIJIJI CHA KILOLELI WILAYANI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeelezwa kuwapatia Elimu ya ujasiri wanawake wa Kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu, na kuamua kujikita kwenye shughuli za ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi na kuachana na utegemezi kutoka kwa waume zao.

Hayo yamebainisha leo Machi 27, 2024 na Wanawake kutoka  Kikundi cha kutengeneza bidhaa za Ngozi cha Kalangale kilichopo Kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Makamu Mwenyekiti wa Kikundi hicho Rejina Emmanuel, amesema awali wanawake kijijini humo walikuwa tegemezi kutoka kwa waume zao pamoja na kukabiliwa na maisha duni kwa sababu walikuwa wa mama wa nyumbani lakini sasa hivi wanajishughulisha na ujasiriamali na siyo tegemezi tena.

“Tunaishukuru TGNP kwa kutupatia elimu ya ujasiri sisi wanawake wa hapa Kiloleli, kwa kweli sasa hivi tunafanya shughuli za kiuchumi pamoja na wanaume kupitia vikundi ikiwamo kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi kama vile Viatu, Mikoba, Mikanda kazi ambazo tulizani niza wanaume peke yao,”amesema Rejina.
Mwanamke mwingine Malta Ngwelu, amesema baada ya kupewa elimu kwamba hakuna kazi ya wanaume wala wanawake na TGNP ndipo wakaamua kuthubutu na kuunda kikundi cha jinsi zote na kufungua Kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi na kujikwamua kiuchumi na kutokuwa tegemezi tena kwa waume zao.

Amesema, Kiwanda hicho kimekuwa lulu kwa wanawake, na hata kuondokana na vitendo vya ukatili vitokanavyo na mfumo dume kutokana na kwamba wamejiimarisha kiuchumi kwa sababu na wao wanajishughulisha na kuingiza kipato katika familia pamoja na kusomesha watoto wao hivyo kuendeleza harakati za mabadiliko katika jamii.

Mjumbe wa kikundi hicho Joseph Soleya, amesema kwamba wamefurahia kufanya kazi pamoja na wanawake sababu ni wachapakazi wazuri wanajituma kujituma na pia waaminifu na kikundi chao tangu kianzishwe hakijawahi kuwa na migogoro.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kiloleli wilayani Kishapu kinachosimamiwa na TGNP, Zacharia Pimbi, amesema baada ya wananchi hao kupewa elimu ya ubunifu na kuibua miradi, ndipo wakaona watumie fursa ya kuanzisha Kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za Ngozi na kuungana jinsi zote.

Amesema kupitia kikundi hicho Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia nchi Vijijini (EBBAR) walikiwezesha kikundi hicho kiasi cha fedha Sh. milioni 95.6 na kuanzisha Kiwanda hicho cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na Ngozi.
“Kikundi hiki kina wanachama 17, wanawake 10 na wanaume 7, na Ofisi ya Makamu wa Rais ilitupatia fedha ili wananchi wajishughulishe na biashara zitokanazo na bidhaa za Ngozi, na kuacha kufanya biashara za kuuza mkaa ili wasikate miti hovyo na kusababisha uharibifu wa Mazingira,” amesema Pimbi.

Aidha, amesema pia Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wameendelea kuwa nao bega kwa bega na hata hapo awali ili kuwapatia fedha za Mikopo ya asilimia 10 Sh. milioni 10 , na kwamba changamoto ambayo inawakabili kwa sasa ni ukosefu wa mashine ya kutengeneza ngozi sababu ‘Material’ huyafuata Jijini Mwanza.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Makamu Mwenyekiti wa Kikundi wakikundi cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na Ngozi Rejina Emmanuel akizungumza na Waandishi wa habari.
Mjumbe wa Kikundi Malta Ngwelu akizungumza na Waandishi wa habari.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kutoka (TGNP) Kiloleli wilayani Kishapu Zacharia Pimbi, akizungumza na Waandishi wa habari.
Shughuli za utengenezaji bidhaa zitokanazo na ngozi zikiendelea.
Wanakikundi wakionesha baadhi ya bidhaa zitokanazo na ngozi ambazo wamezitengeneza .
Wanakikundi wakionesha baadhi ya bidhaa zitokanazo na ngozi ambazo wamezitengeneza .
Muonekano wa baadhi ya bidhaa za viatu vilivyotengenezwa na Ngozi na Kikundi hicho.
Muonekano wa baadhi ya viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi na kikundi hicho.
Muonekano wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.

Post a Comment

0 Comments