Header Ads Widget

SHINYANGA EVAWC WORKING GROUP WAPONGEZWA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO,KONGAMANO LA MAFANIKIO MWAKA 2023

SHINYANGA EVAWC WORKING GROUP WAPONGEZWA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO,KONGAMANO LA MAFANIKIO MWAKA 2023

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MUUNGANO wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Shinyanga, (Shinyanga Ending Violence Against Women and Children Working Group “EVAWC”), ambayo yanafanya kazi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, wamepongezwa kwa kupunguza matukio ya ukatili ndani ya jamii zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Pongezi hizo zimetolewa leo March 1,2024, kwenye Kongamano la Mwaka la kutafakari Mafanikio na Mwenendo wa Utekelezaji wa Shughuli za Shinyanga EVAWC Working Group, kwa mwaka 2023 na kupendekeza nini kifanyike kwa mwaka 2024.


Mgeni Maalumu kwenye Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, amewahidi kwamba kutokana na kazi kubwa ambayo wanaifanya, Serikali itaendelea kuwa nao bega kwa bega katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, na milango iko wazi na pale penye Changamoto wasisite kuwasiliana naye.
Amesema Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake ndiyo maana kuna Mashirika yasiyo ya Kiserikali,ambayo yanasaidizana kutatua Changamoto mbalimbali ndani ya Jamii yakiwamo masuala ya ukatili wa kijinsia na kuupongeza umoja wa Mashirika Shinyanga kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya.

“Kidole kimoja hakivunji chawa,umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, suala la ukatili ni mtambuka linatakiwa kuhusisha Taasisi tofauti tofauti kama mnavyo fanya nyie Shinyanga EVAWC ili kuwe na nguvu na sauti ya pamoja katika kutokomeza ukatili,”amesema Samizi.
“Mimi ni mdau namba moja wa kupinga vitendo vya ukatili na ninapokea simu muda wote na taarifa za ukatili ambazo napatiwa hua nazifanyia, na kazi ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya ni pamoja na kupokea taarifa za Mashirika yasiyo ya Kiserikali, hivyo mana karibishwa muda wote tufanye kazi na kuleta ukombozi kwa jamii,”ameongeza.

Aidha, amesema Serikali pamoja na Mashirika yapo katika safari moja ambapo kitu kubwa wasiachane bali washikamane katika utatuzi wa Changamoto mbalimbali ndani ya Jamii na kwamba Mafanikio hayo ambayo leo wana sherehekea bila ya kuwa na nguvu ya pamoja wasingefika hapo kupunguza ukatili ndani ya jamii.
Katika hatua nyingine ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi malezi bora ya watoto wao na wasiwe bize na maisha ikiwamo kuchezea simu za mkononi na kwamba hata kama Mtoto kafanyiwa ukatili akitaka kumueleza mzazi wake anashindwa sababu yupo bize akichezea simu.

“Wazazi wa siku hizi hawana hata Sensi wala kutafsiri vilio vya watoto wao, zamani mtoto akilia mzazi unajua atakuwa na tatizo Fulani siku hizi hakuna, watu wako bize na maisha na hata akikuta Mtoto wa jirani anafanyiwa ukatili akemei kitendo hicho ndiyo kwanza anapiga picha, wazazi badilike msiwe chanzo cha kufanyia ukatili watoto, Amesema Samizi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Shinyanga Aisha Omary ambaye pia ni Mratibu wa MTAKUWWA wilayani humo, ameyapongeza Mashirika hayo kwa kusaidiana na Serikali kupunguza ukatili ndani ya Jamii zikiwamo Ndoa za Mimba za utotoni,huku akiahidi Serikali itaendelea kushirikiana nao pamoja na kuweza Mazingira wezeshi ya kufanya kazi zao bila ya mkwao wowote.

Mwakilishi wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Shinyanga Takelove Ayo, amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali kupitia umoja wao Shinyanga EVAWC wamekuwa wakifanya kazi kubwa na hata kuisaidia Polisi katika kesi za ukatili ambapo zinakwenda kwenye dawati hilo zikiwa zimekamilika na watuhumiwa wengi wamefungwa Jela.
Neema Msangi kutoka Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) ambao ni miongoni mwa wafadhiri kwa kuyawezesha mashirika hayo kufanya kazi ya kutokomeza ukatili dani ya jamii, wamesema wamefarijika kwa kazi ambayo wanaifanya kupitia umoja wao na mafanikio yameonekana ambapo ukatili umepungua ndani ya jamii siyo kama zamani.

Naye Mwenyeki wa Shinyanga EVAWC Working Group Jonathan Manyama, amesema umoja huo wa Mashirika waliuanzisha Mwaka 2021 wakiwa na wanachama 15, mwaka 2022 wakafika 28 na sasa wapo 36, na kwamba umoja huo haupokei Mashirika tu bali hata Mtu Mmoja, ili kuendelea mapambano ya kutokomeza ukatili.
Amesema malengo ya kuanzisha umoja huo ni kuunganisha nguvu na kuwa na sauti ya pamoja katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Mkoa wa Shinyanga tulikuwa wakwanza kwenye masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni lakini sasa hivi ukatili umepungua na tupo nafasi ya 10 siyo namba moja tena,”amesema Manyama.
Aidha,Kwa mujibu wa Takwimu ambazo zimetolewa na Tanzania Demographic Health Survey (TDHS) mwaka 2022, Mkoa wa Shinyanga umepunguza tatizo la mimba za utotoni kutoka asilimia 34 hadi 21 ikiwa ni moja ya jitihada ambazo zimefanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Kauli Mbiu kwenye Kongamano hilo inasema kuchochea Mabadiliko, Kuimarisha Jitihada za pamoja ili kuondokana na Mifumo Kandamizi inayochochea ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Shinyanga EVAWC Working Group Jonathan Manyama akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Shinyanga EVAWC Working Group Jonathan Manyama akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO Gerald Ng'ong'a akitoa salam za mshikamano kwenye Kongamano hilo.
Sabrina Majikata kuto ICS akiongoza Majadiliano katika Mada ya Mila na Desturi Kandamizi kwenye Kongamano hilo jinsi zinavichangia ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Mama Karena akitoa akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Damari Mollessy akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Veronica Masawe akiongoza Mada ya Safari ya Mafanikio chini ya nguvu za pamoja kwenye Kongamano hilo.
Neema Msangi kutoka WTF-Trust akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Neema Msangi kutoka WTF-Trust akizungumza kwenye Kongamano hilo.
MC Mama Sabuni akisherehesha Kongamano hilo.
Mussa Ngangala kutoka TVMC akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Peter Amani akiongoza Mada kwenye Kongamano hilo.
Peter Amani akiongoza Mada kwenye Kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mada ya Mila na Desturi ikijadiliwa kwenye Kongamano hilo.
Wanafunzi wakitoa Igizo lenye ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili kwenye Kongamano hilo.
Mada mbalimbali zikiendelea kujadiliwa kwenye Kongamano hilo.
Mada mbalimbali zikiendelea kujadiliwa kwenye Kongamano hilo.
Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Keki ikikatwa kwenye Kongamano hilo.
Muonekano wa Keki.
Mwenyekiti wa Shinyanga EVAWC Working Group Jonathan Manyama (kushoto)akimlisha Keki Mratibu wa WTF-Trust Mkoa wa Shinyanga Groly Mbia.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Zoezi la kulishana keki likiendelea.
Vyeti vya pongezi vikitolewa kwa wanawake vinara wa ukatili ngazi ya jamii.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa kwa wanawake vinara wa ukatili ngazi ya jamii.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa kwa wanawake vinara wa ukatili ngazi ya jamii.
Vyeti vya pongezi vikiendelea kutolewa kwa wanawake vinara wa ukatili ngazi ya jamii.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.

Post a Comment

0 Comments