
   DC- Kishapu akiwa na  wataalamu na viongozi wa dini
 Na Kareny Masasy,
OFISI  ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la ICS imetoa 
utambulisho wa namna ya utekelezaji wa mpango wa Jumuishi wa Taifa  Makuzi,Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto   (PJT MMMAM) kwa viomgozi 
na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu pamoja na Ofisi ya Mkuu
 wa Wilaya Kishapu ili waweze kuwafikisha watoto kwenye
 ukuaji timilifu.
 Akiwasilisha
 programu hiyo  leo  Afisa  ustawi wa jamii   kutoka mkoani Shinyanga 
Lyidia Kwesigabo  alisema  ili mtoto aweze kufikia hali nzuri ya ukuaji 
bado ni lazima  kusimamiwa kwenye nguzo tano  ambazo ni Afya,Lishe bora,
 Ujifunzaji wa awali,Malezi yenye mwitikio na ulinzi na Usalama.
Kikao
 hicho kiliratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa 
kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la  investing in Children 
and Strengtherning  their Societies (ICS) nakuhudhuriwa na viongozi 
pamoja na wataalamu wa idara mbalimbali ambapo  Lydia Kwesigabo 
alisema jamii inatakiwa ipate elimu hii muhimu kwa ujumuishi wake kwa 
faida ya watoto familia na Taifa kwa ujumla. 
 
Kwesigabo
 amesema programu hiyo ilizinduliwa mwezi Desemba 2021 na ni programu ya
 miaka mitano 2021/2022  hadi 2025/2026  ambayo imelenga watoto kuanzia 
umri wa mwaka  0 hadi miaka ( 8) ambao ni umri  uko katika hatua ya 
ukuaji.
“Kwesigabo  
amesema  kuhusu dhana za ujifunzaji zinaweza kuandalliwa kulingana na 
mazingira huskika kwa kutumia vitu vya asili na zikatumika katika vituo 
vya Kulelea watoto wadogo mchana na shule za awali.
  
Kwesigabo
 amesema  nguzo zote 5 ni  muhimu kwa watoto na pia  mama anapokuwa 
mjamzito hatakiwi kuwa na msongo wa mawazo na pia baba na mama 
wanatakiwa wamsemeshe mtoto aliyeko tumboni  kwani pia husaidia mtoto 
kukua tumboni akiwa na furaha na uchangamshi mzuri na Ubungo kuendelea 
kukua vizuri
Mgeni rasmi 
ambaye ni  Mkuu  wa wilaya  ya Kishapu Joseph Mkude amesema programu 
hiyo ataisimamia vizuri hata kwenye ngazi za vijiji na kata kuhakikisha 
watoto wanakuwa katika mazingira Bora.
 
"Kuna
 baraza la madiwani kesho kutwa nitazungumza programu hiyo kwa madiwani 
ili waweze kuuelewa na hakuna kitakacho shindikana  watumia rasilimali 
zilizopo kwenye maeneo Kama alivyosema  afisa ustawi wa jamii"amesema 
Mkude.
Mkurugenzi wa 
halmashauri hiyo Emanuel Jonson amesema  programu hiyo imekuja 
wameipokea watatekeleza huku sheikhe  kutoka Kishapu  Adamu Nkhambi 
alisema wanaume wanafikiri wakiweka ujauzito inatosha kumbe Kuna Malezi 
zaidi yanahitajika ili mtoto aweze kukua vizuri na mwenye maadili.
Mwenyezi
 Mungu  katika vitabu  vyake  amesema kazaeni mjaze dunia tafsiri yake  
kwenye Malezi  wanaume  na wanawake wawajibike  utakuta mama anaenda 
mwenyewe kliniki wakati wa ujauzito hadi  anajifungua ,Malezi ya watoto 
yukoi peke yake  hivyo kama Viongozi wa Dini wataendelea kuelimisha 
waumini wao juu ya programu hii
 Mkuu  wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akishika toleo la kitabu cha  PJT-MMMAM.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude  akisikiliza utambulisho wa  PJT-MMMAM

Sheikhe   Adamu Nkhambi kutoka kishapu akichangia mada kuhusu PJT-MMMAM

Mkuu wa wilaya akiwa na viongozi wa dini.


 
                Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464