Header Ads Widget

RC MNDEME AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA SUKARI SHINYANGA

RC MNDEME AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA SUKARI SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Sukari mkoani Shinyanga, kuona ni changamoto zipo ambazo zinasababisha washindwe kuuza Sukari kwa bei elekezi ya Serikali.
Kikao hicho kimefanyika leo Februari 27,2024.

Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga kuna tatizo la bei ya Sukari kutokuwa Rafiki wa walaji, hivyo ameona akutane na Wafanyabiashara hao ili kuzungumza nao tatizo ni nini wameshindwa kuuza Sukari kwa bei elekezi ya Serikali.

Amesema Serikali imetoa maelekezo ya bei elekezi kwa kila Kanda, ambapo Kanda ya Ziwa ukiwamo Mkoa wa Shinyanga, kwamba bei ya Jumla jumla ni Sh. 2,600 hadi 2,800, Rejareja Sh. 2,800 hadi 3,000, na kwamba Mlaji wa Sukari kwa Mkoa huo wa Shinyanga anauziwa Sukari Kilo moja Sh. 3,200 hadi 5,000.
“Kunanini kwa wafanyabiashara mnashindwa kuuza Sukari kwa bei elekezi ya Serikali, mnaficha Sukari kwanini, mpaka tunafikia hatua ya kukamatana, na mpaka sasa tumewakamata wafanyabiashara Sita kutoka Kahama, Watatu wakubwa, Watatu wadogo kwa kwenda kinyume na maelekezo ya Serikali ya kuuza Sukari kwa bei isiyo elekezi,”amesema Mndeme.

“Hii kamatana kamatana, vutana vutana, nikaona hapana ngoja tukae tuzungumze tujua kwanini wafanyabiashara hawa wanauza Sukari kinyume na bei elekezi, kwanini wanaficha Sukari, kwanini hawaendi kununua Sukari, ndipo nikaona tukutane tuongee lasivyo tutawakamata wote,”ameongeza Mndeme.
Amesema Serikali imetoa Ushuru kwenye Sukari “Impot duty” asilimia 35, VAT asilimia 18 ili bei iwe rafiki, laki bei haishuki ipo vile vile huku wilaya ya Kahama kukiwa hakuna Sukari, tofauti na Kishapu na Shinyanga.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wamesema kwamba tatizo siyo wao ambao wanasabisha bei ya Sukari kuwa juu, bali ni kwenye Viwanda na Maeneo ambayo wanauziwa Sukari hiyo, kuwa bei elekezi ya Serikali haiendani na uhalisia wa bei ya Sokoni ambayo wananunua Sukari.
Wametolea Mfano kwamba Mfuko wa Sukari Kilo 25 bei elekezi ya Serikali inasema uuzwe kwa Sh. 70,000 lakini wao wanauziwa Sh.75,500, na kutoa ushauri kwa Serikali kwamba wanapopanga bei elekezi washirikishe wamiliki wa Viwanda na wafanyabiashara, ushauri ambao Mkuu wa Mkoa ameahidi kuufanyia kazi.
Wafanyabiashara wa Sukari wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Wafanyabiashara wa Sukari wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Wafanyabiashara wa Sukari wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.

Post a Comment

0 Comments