Header Ads Widget

KATAMBI HASHIKIKI KWA MAENDELEO SHINYANGA,AKABIDHI "AMBULANCE",VITANDA HOSPITALI YA MANISPAA YA SHINYANGA


KATAMBI HASHIKIKI KWA MAENDELEO SHINYANGA, AKABIDHI AMBULANCE,VITANDA HOSPITALI YA MANISPAA YA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amesifiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi,kutokana na kuleta Maendeleo makubwa Shinyanga chini ya Daktari Rais Samia Suluhu Hassan.
Pongezi hizo zimetolewa leo Februari 8, 2024 kwenye hafla ya Mbunge Katambi ya kukabidhi Gari la Wagonjwa(Ambulance) na Vitanda katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,pamoja na kugawa Majiko ya Gesi kwa Watumishi mbalimbali wa Serikali.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza kwenye hafla hiyo, amesema Katambi amefanya mambo mengi ya kimaendeleo katika Jimbo hilo la Shinyanga ambapo mengine hayapo hata kwenye ahadi zake.
“Katambi umefanya mambo mengi ambayo hayapo hata kwenye ahadi zako,”amesema Makombe.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo, amempongeza Mbunge Katambi kwa kuchapa kazi na kuwatumikia wananchi, ikiwamo utoaji huo wa gari la wagonjwa na kuboresha huduma za afya.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amemshukuru Mbunge huyo kwa kutoa gari la wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, ambayo kwa sasa imefanyiwa maboresho makubwa na gari hilo lilikuwa na uhitaji mkubwa

Chifu Njange Jidola wa pili, amempongeza Katambi kwa kujali afya za wananchi wake na kukabidhi gari hilo la wagonjwa pamoja na Vitanda, na kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya katika maeneo mbalimbali na kuokoa afya za wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Revocatus Rutunda, amesema wanashukuru kupewa gari hilo la wagonjwa ambapo ilikuwa changamoto kubwa katika Hospitali ya Manispaa hiyo.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk. Elisha Robert, amesema katika Manispaa hiyo uhitaji wa Magari ya wagonjwa ni Manne, kwamba kulikuwa na Magari Mawili lakini Moja liliharibika na kusalia Moja, hivyo kupata gari hiyo imekuwa mkombozi kwa wagonjwa.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi gari hilo na vitanda vya wagonjwa, ameema hiyo ni sehemu ya ahadi zake katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Amesema ndani ya miaka mitatu ya kipindi chake cha Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini, amefanya mambo mengi ya kimaendeleo na hata kupitiliza ahadi ambazo alikuwa ameahidi kipindi cha Kampeni kwenye uchaguzi mkuu uliopita 2020, na bado anaendelea kuwatumikia wananchi ikiwamo uboreshaji wa huduma za afya.
“Gari hili la wagonjwa ambalo nalikabidhi ni moja ya vitendea kazi muhimu katika Sekta ya Afya, kwa kubeba wagonjwa na kuwa wahisha kupata huduma za matibabu na kuokoa Afya zao,”amesema Katambi.

Amesema katika Utawala wake wa Ubunge ataendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora za Afya chini ya Daktari Rais Samia ikiwamo upatikanaji wa Vifaa Tiba, Madawa pamoja na kumalizia ujenzi wa Maboma ya Zahanati ili ya anze kutoa huduma kwa wananchi.
Nao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga akiwamo Eliza Masanja, amesema upatikanaji wa Magari ya wagonjwa ni muhimu sana hasa kwa akina Mama Wajawazito, kuwa wahisha kupata huduma za kujifungua kwa uharaka na kuokoa maisha ya Mama na Mtoto, huku akimpongeza Katambi kwa kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha, kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa gari la wagonjwa na vitanda, yametolewa pia Majiko ya Gesi kwa Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Walimu, Wakuu wa Idara na Watumishi wa Afya.

TZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Gari la Wagonjwa na Vitanda katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na Majiko ya Gesi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Gari la Wagonjwa na Vitanda katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na Majiko ya Gesi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Anorld Makombe akizungumza kwenye hafla hiyo.
Chifu Njange Jidola wa pili akizungumza kwenye hafla hiyo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Revocatus Rutunda akizungumza kwenye hafla hiyo.
Viongozi Meza Kuu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakishuhudia Makabidhiano ya gari la wagonjwa la Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akikata Utepe kukabidhi gari la wagonjwa la hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Katambi akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe kwenye gari hilo la wagonjwa la hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Katambi akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe kwenye gari hilo la wagonjwa la hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Muonekani wa gari la wagonjwa la hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Katambi akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Revocauts Rutunda Vitanda vya hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Hafla ikiendelea ya makabidhiano ya vitanda.
Makabidhiano Majiko ya Gesi yakiendelea.
Makabidhiano Majiko ya Gesi yakiendelea.
Makabidhiano Majiko ya Gesi yakiendelea.
Makabidhiano Majiko ya Gesi yakiendelea.
Majiko ya Gesi.

Post a Comment

0 Comments