Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imewakumbuka watu wasiojiweza katika Manispaa ya Shinyanga kwa kuwapa zawadi za mwaka mpya ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Na Ofisi ya Mahusiano,SHUWASA.
Zawadi hizo zimetolewa jana Desemba 30, 2023 zikijumuisha Mchele, Mafuta ya kupikia,Sukari na Sabuni.
ambapo jumla ya wasiojiweza 13 wamepatiwa zawadi hizo kila mmoja akipatiwa Mchele kilo tano, Sukari kilo mbili, Mafuta ya kula Lita tatu na Sabuni miche miwili.
SHUWASA imekuwa ikiwasaidia watu hao wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na kuwalipia bili za maji za kila mwezi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Watu wenye uhitaji wakiendelea kupewa zawadi na SHUWASA.
zawadi ya vyakula.
Watu wenye uhitaji wakiendelea kupewa zawadi na SHUWASA.
Watu wenye uhitaji wakiendelea kupewa zawadi na SHUWASA.
Mtumishi wa SHUWASA akiwa amebeba Mafuta ya Kula.
Watu wenye uhitaji wakiendelea kupewa zawadi na SHUWASA.
Watu wenye uhitaji wakiendelea kupewa zawadi na SHUWASA.
Pictures edited by Marco Maduhu.
0 Comments