Header Ads Widget

WAZIRI WA ARDHI JERRY SILAA AFANYA ZIARA MKOANI SHINYANGA ATAKA UTATUZI MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi Jerry Silaa amewataka Watumishi wa Ardhi mkoani Shinyanga kutatua Migogoro ya Ardhi

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa, amewataka Watumishi wa Ardhi mkoani Shinyanga, kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kutatua Migogoro ya Ardhi, na kwamba siku Rais Samia akifanya ziara katika Mkoa huo asipokelewe na Mabango ya Migogoro ya Ardhi, bali apokelewa kwa shangwe kwa kupungiwa mikono kwa furaha na siyo mabango.
Amebainisha hayo leo Decemba 4, 2023 wakati alipofanya ziara mkoani Shinyanga ya kuzungumza na Watumishi wa Ardhi na Viongozi mbalimbali, huku akipokea Malalamiko ya Mgogoro wa kugombea mpaka katika machimbo ya madini yaliyopo Kijiji cha Chang’ombe Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Nyan’ghwale mkoani Geita.
Amesema Watumishi wa Ardhi wanapaswa kubadilika katika utendaji wao kazi katika kutatua migogoro ya ardhi, na wale ambao hawataweza kuendana na kasi yake ni vyema wakapisha sababu wamechoka kila anaposimama kiongozi mkubwa kuzungumza lazima aionyeshee kidole Wizara ya Ardhi kuwa ni tatizo.

“Kazi niliyopewa kufanya na Dk. Samia ni kuhakikisha kwamba siku akifanya ziara hapa Shinyanga akipita barabarani wananchi wawe wanampungia mikono, ni fedheha kubwa anapokuja kwenye ziara Mheshimiwa Rais badala ya wananchi kumpungia mikono kwa furaha wanashika Mabango, kushika kwao Mabango ina maana kwamba sisi aliotupa dhamana kumsaidia hutufanya kazi yetu,”amesema Waziri Silaa.
Aidha, akizungumzia utatuzi wa Mgogoro wa Mpaka wa eneo la Mchimbo katika Kijiji cha Chang’ombe Halmashauri ya wilayani Shinyanga na Nyan’hwale mkoani Geita, amesema Mgogoro huo hadi kufikia Decemba 14 mwaka huu utakuwa tayari ameutatua na kuweka alama za mipaka.

Amesema kuanzia leo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mkurugenzi wa upimaji wa Ramani na Msajiri wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba, kwamba ndani ya siku saba wawe wameshafika kwenye eneo hilo la Mgogoro huo wa mpaka ili kufuatilia utatuzi wake, na kabla ya Decemba 14 wawe wameshampatia taarifa na kisha yeye kuja kuweka mipaka na kuutatua.
Awali akitoa Malalamiko ya Mgogoro huo wa Mpaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, amesema kumekuwa na Mgogoro wa kugombea mpaka katika eneo la machimbo ya dhahabu kijiji cha Chang’ombe baini ya Halmashauri hiyo na wilaya ya Nyan’hwale na kumuomba Waziri autatue.

Amesema Mgogoro huo umekuwa na Sintofahamu akidai kwamba Ofisi ya Madini kutoka mkoani Shinyanga wamekuwa wakikusanya mapato kwenye machimbo hayo, lakini Mapato ya Halmashauri yamekuwa yakienda Nyang’hwale mkoani Geita, na Mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na kuikosesha Mapato Halmashauri.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema licha ya kuendelea kutatua Migogoro mbalimbali ya Ardhi mkoani humo, amemuomba Waziri huyo wa Ardhi kuwasaidia kuutatua Mgogoro huo wa Mpaka baina ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Nyan’hwale sababu upo chini ya uwezo wa Wizara hiyo.

Amesema Serikali mkoani Shinyanga wataendelea kusimamia suala la mipango miji pamoja na matumizi bora ya ardhi ili kuzuia matatizo ya Migogoro ya ardhi yasiendelee kuibuka.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Jerry Silaa akizungumza kwenye kikao mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akizungumza kwenye kikao hicho.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Jerry Silaa (kushoto)akipokea taarifa ya Ardhi kutoka kwa Kamishina msaidizi wa Ardhi mkoani Shinyanga Leo Komba.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments