Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAJIONEA MAAJABU YALIYOMO KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUBONDO


Suzy Luhende Shinyanga Press blog


Watanzania wameshauriwa  kutembelea hifadhi ya Taifa ya Rubondo iliyopo katika Mkoa wa Geita na Kagera ambayo inavivutio vingi vya asili  wakiwemo Tembo, Twiga, swala, Sitatunga, ndege kasuku, Sokwe,nguruwe pori, mamba na wanyama mbalimbali wamo katika hifadhi hiyo.

Ushauri huo ameutoa mhifadhi mwandamizi na mkuu wa kitengo cha uhasibu, ambaye amekaimu nafasi ya mkuu wa hifadhi katika kisiwa kikubwa cha Rubondo Anold Mwasuluka  wakati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliotembelea hifadhi hiyo, ambaye amewashauri watanzania wafanye utalii wa ndani ili kujionea wanyama wa asili waliomo katika kisiwa hicho.

Mwasuluka amesema katika kisiwa hicho kuna wanyama wa asili na walioletwa, hivyo watanzania wakitembelea watajionea wenyewe wanyama mbalimbali kwa gharama nafuu ambapo gharama za watalii wa ndani ni sh 5900 na maradhi sh 30,000, kwa mwaka wanapata watalii zaidi ya 3000.ikiwa watalii wa nje wakikitoa gharama za dola 30.

"Kuna njia tatu za kufika Rubondo njia ya kutumia maji ni boti za kukodisha, pia kuna njia ya anga tunatumia ndege, njia ya barabara kupitia Geita mjini, na tuna wanyama wa asili na walioletwa sitatunga ngurue pori twiga tembo baadhi ya ndege kasuku ambao waliletwa toka mwaka  2000 katika eneo la uhifadhi tunawakaribisha sana" 

"Pia moja ya watalii wakubwa katika kisiwa hiki ni watalii wazawa tunaishukuru serikali ya Tanzania imekuwa ikihamasisha sana, hivyo watanzania wamehamasika kwa kiasi kikubwa baada ya Rais Samia Suluhu  kuanzisha utalii wa ndani watanzania wanakuja kwa wingi wengi wafanyabiashara kutoka Geita, Mwanza na Kahama, wanafunzi na wengine kutoka nje ya nchi, kuna mapumziko mazuri yametulia"ameongeza.

Afisa uhifadhi ambaye pia anashughulikia kitengo cha ujirani mwema Robert Forcus Mushi amesema katika kila shughuli akija mtu mmoja inakuwa gharama kidogo,hivyo wakiwa wengi gharama inakuwa nafuu, na kiwango cha mtalii wa kutoka nje ni dola 30.

Aidha mtalii wa ndani anatozwa gharama ndogo sh 5900, huku kitengo cha ujirani mwema wakitoa elimu ya uhifadhi, mashuleni, wanafundisha vijana ili wajue uhifadhi na waupende.

Amesema katika kitengo cha ujirani mwema wameanzisha  miradi mbalimbali ya shule ufugaji nyuki upandaji miti na miradi mingi mbalimbali  zikiwemo zahanati na kuwahamasisha vijana kuupenda utalii wa ndani waweze kutembelea mali asili yao kwa gharama kidogo.

"Kuna uvuvi wa kitali,i utalii wa sokwe ni utalii mkubwa zaidi Rubondo wageni wanaona sokwe  tofauti kuna sokwe anaitwa dogo janja anabembea kwenye kamba anacheza akiona wageni anafurahi, kuna sokwe  Msukuma ambaye alipewa jina baada ya Mbunge Msukuma kutembelea katika hifadhi hiyo "amesema Mushi.

Kwa upande wake mwongoza watalii katika hifadhi hiyo Samweli Stephano John amesema katika hifadhi hiyo kuna ndege huwa wanakuja kutoka nchi ya marekani kwa ajili ya likizo kuanzia kipindi cha mwezi june mpaka septemba ambao wanajega kiota, hivyo watalii wanavutiwa sana na ndege hao.

"Katika kisiwa hiki walikuwa wakiishi wazinza na kufanya shughuli zao mbalimbali za kiimani na walikuwa wakiamini kwamba kama kuna mtu amezaa mapacha ni mkosi ama akizaliwa albino ndio wanaenda kwenye eneo la maji matakatifu kufanya matambiko yao ili kuondoa mikosi hiyo"amesema John.

"Kati kisiwa hiki pia kuna sehemu ya maji matakatifu na kuna sehemu kuna chungu ambacho kiliwekwa na waanzilishi ambao walikuwa wa kabila la wazinza walikuwa wakienda kujiungamanisha pale wanapokuwa na mahitaji yao mbalimbali ambacho hata sasa wanafunzi wengi wanafika pale na kufanya maombi yao ama kuandika barua ya kuomba wafanikiwe katika masomo yao"ameongeza John.

Amesema wanyama wa kuletwa kama twiga, swala tembo walianza kupelekwa katika kisiwa hicho mwaka 1965 wakati likiwa ni pori la akiba walikuwepo falu waliwindwa na wakaisha, hivyo kwa sasakuna ulinzi mkali katika hifadhi hiyo hairuhusiwi kuvuna mali za hifadhi 

Baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea katika hifadhi hiyo akiwemo Chibura Makorongo amesema amesema amefurahia utalii wa ndani, kwani alikuwa hajafika katika hifadhi hiyo, hivyo amejionea wanyama mbalimbali wakiwemo samaki wakubwa sangala na Sato ambao wanaishi majini.

Mhifadhi mwandamizi na mkuu wa kitengo cha uhasibu, ambaye amekaimu nafasi ya mkuu wa hifadhi katika kisiwa kikubwa cha Rubondo Anold Mwasuluka akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho

Afisa uhifadhi katika hifadhi ya Rubondo ambaye pia anashughulikia kitengo cha ujirani mwema Robert Forcus Mushi akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika kisiwa hicho

Afisa uhifadhi katika hifadhi ya Rubondo ambaye pia anashughulikia kitengo cha ujirani mwema Robert Forcus Mushi akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika kisiwa hicho
Mwongoza watalii katika hifadhi hiyo Samweli Stephano John akionyesha chungu kilichokuwa kikitumiwa na wazinza waliokuwa wakienda kujiungamanisha kikiwa ndani ya hifadhi hiyo
Waongoza watalii katika hifadhi hiyo wakiwa ndani ya boti wakitoa maelekezo 
Eneo la maji matakatifu walikokuwa likiwa ndani ya hifadhi hiyo
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ndani ya boti wakiendelea katika kufanya utalii wandani katika kisiwa cha Rubondo
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ndani ya boti wakiendelea katika kufanya utalii wandani katika kisiwa cha Rubondo
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuingia kwenye boti
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuingia kwenye boti

Karibu Rubondo ujionee mwenyewe maajabu yaliyopo utapenda waliotembelea wanaeleza

Post a Comment

0 Comments