Header Ads Widget

RC MNDEME ATEMBELEA UJENZI SKIMU YA UMWAGILIAJI KATA YA NYIDA WILAYANI SHINYANGA

RC MNDEME ATEMBELEA UJENZI SKIMU YA UMWAGILIAJI KATA YA NYIDA WILAYANI SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ametembelea kuona Maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Nyida wilayani Shinyanga, na kuagiza ujenzi huo ukamilike kwa wakati ili wakulima waanze kunufaika nao.

Amebainisha hayo leo Novemba 25,2023 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Skimu hiyo, akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, na kueleza kuwa Kilimo cha uhakika kwa sasa ni Kilimo cha Umwagiliaji.
Amesema anampongeza Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji, na katika Mkoa wa Shinyanga ametoa zaidi ya Sh.bilioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji, ikiwamo ya Kata ya Nyida ambayo imegharimu Sh.bilioni 11.1, na kuagiza ikamilike kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na kufanya kilimo chenye tija kwa kulima mazao ya mpunga.

“Nimekagua Maendeleo ya ujenzi huu wa Skimu ya Umwagiliaji kasi yake hairidhishi kabisa, naagiza hadi kufikia Julai mwakani mradi huu uwe tayari umekamilika, na wananchi waanze kuutumia kwa shughuli za Kilimo na kuongeza uzalishaji wa zao la Mpunga na hata kuinuka kiuchumi na Taifa kwa ujumla, sababu mtakuwa mnalima msimu mzima,”amesema Mndeme.
Nao baadhi ya Wakulima wa zao la Mpunga Kata hiyo ya Nyida akiwamo Paulo Shija, wamempongeza Rais Samia kwa kuwatekelezea mradi huo wa Kilimo cha Umwagiliaji, ambapo watakuwa wakilima mara mbili kwa msimu mmoja na kufanya kilimo chenye tija.

Naye Msimamizi wa Mradi huo wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida Sifa Revocatus, akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amesema ulianza kujengwa Januari 11 Mwaka huu ambapo muda wa Mkataba ni siku 540 na kwamba utakamilika Julai 4 mwakani 2024.
Amesema mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi SIETCO JV JGV, kwa gharama ya Sh.bilioni 11.1 fedha kutoka Serikali kuu kupitia Bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka wa fedha 2022/2023, na utakapo kamilika utamwagilia mashamba ya Mpunga Hekta 421 kwa Wakulima 350 pamoja na kunyweshea mifugo, na kuahidi kuukamilisha ndani ya muda wa Mkataba.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akitoa maelekezo kwa Makandarasi juu ya ujenzi wa Skimu hiyo ya Mwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akiangalia Ramani ya ujenzi wa Skimu ya Mwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akisikiliza maelezo ya utekelezaji wa ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkandarasi Han Zhen Liethng akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga juu ya utekelezaji wa ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Ujenzi Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida ukiendelea.
Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ukiendelea.
Ukuta wa Skimu ya Umwagiliaji.
Mtambo wa ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Ujenzi wa Skimu ya Umwagilija ukiendelea Kata ya Nyida.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Nyida wilayani Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments